Tangu kutangazwa habari kuwa mchezaji wa Tanzania (Zanzibar) Adam Nditi kusajiliwa na klabu ya Chelsea kama mchezaji wa kulipwa, mengi yameanza kujulikana kutoka kwake.
Nditi ambaye ni mtumiaji mzuri wa mtandao wa Twitter ameonesha kuwa pamoja na kukaa chini Uingereza tangu mwaka 2008, hajasahau muziki wa nyumbani.
Katika swali aliloulizwa na miongoni mwa watu wanaomfuata kwenye Twitter aliyetaka kujua ni kitu gani ambacho husikiliza kabla ya mechi ili kupata mzuka, alijibu husikiliza Bongo Flava.
Ni jambo zuri kuona bado anazifeel flava za nyumbani ambazo bila shaka humwongezea morali kwa kumkumbusha kuwa nyuma yake kuna watanzania kibao ambao si ndugu zake tu, wanaomwembea dua kila kukicha ili aendelea kufanikiwa zaidi.


No comments:
Post a Comment