Timu ya Oklahoma City Thunder iliyoingia fainali mwaka huu kwenye ligi ya kikapu nchini Marekani NBA msimu ulioisha imekubali kuingia mkataba wa miaka miwili na mchezaji wa Tanzania Hasheem Thabeet.
Thunder itakuwa ni timu ya nne kwa Thabeet, 25, tangu achukuliwe mwaka 2009 kwenye NBA Draft.
Mtanzania huyo mwenye urefu wa 7-foot-3 anashikilia rekodi hafifu ya wastani wa pointi 2.2 na rebounds 2.7 kwenye misimu mitatu akiwa na Memphis Grizzlies, Houston Rockets na Portland Trail Blazers.
Hata hivyo Thabeet atajikuta akikaa benchi mara nyingi kwakuwa Thunder, itawachukua pia wachezaji wakali kama Kendrick Perkins, Serge Ibaka, Nick Collison na Cole Aldrich msimu ujao.
Pia kwa mujibu wa makala ya mwandishi wa mtandao wa
kansascity.sbnation.com, Matt Conner amemponda Hasheem kwa makala yake ‘NBA Free Agency Rumors: Hasheem Thabeet To Thunder Should Not Excite Anyone’
Anasema, “Thabeet siku zote ameonesha kuwa zezeta mno ili kumruhusu kucheza dakika kadha kwa level za NBA.”
“Hiyo inamfanya Thabeet kuwa na mashaka kama atakuwa na muda wa kucheza akiwa na Oklahoma City Thunder.”
“Memphis Grizzlies huenda walifanya blunder kubwa zaidi kwenye historia ya NBA Draft kwa kumchukua Thabeet kama No. 2 mwaka 2009.”
Ameendelea kuandika, "na kwa utamaduni wa Thunder unaohusisha maendeleo na kukua, labda mwishowe Thabeet anaweza kugundua kipaji kidogo alichonacho.”
“He just hasn't had the kind of work ethic necessary to make it in the NBA.”


No comments:
Post a Comment