Jitihada za Ustaadh Juma wa Watanashati kumtaka Tundaman awatose Tip Top Connection na ajiunge naye zimegonga mwamba.
Hiyo ni baada ya Tundaman kumwambia ili ajiunge na Watanashati ni lazima aweke mezani dau la shilingi Milioni 100 cash!!!
Akiongea leo na East Africa Radio kwenye kipindi cha Power Jams, Tunda amesema Ustaadh Juma ameshamtumia watu zaidi ya wanne kumpelekea ujumbe wake uliokuwa ukimpa ofa ya shilingi milioni 10 ili ajiunge na Dogo Janja, Suma Mnazaleti na wasanii wengine kwenye kambi yake ya watanashati.
Tunda amesema Ustaadhi huyo amepitia kwa watu wengi akiwemo producer wake Manecky ili wamamshawishi ajiunge na watanashati.
Amedai kuwa kama kweli wana nia ya kumchukua basi wampe dau hilo ili ahakikishe kuwa anagawa kiasi kwa Babu Tale, Abdul Bonge wa Tip Top na familia yake ili aweze kuondoka kiroho safi.
Amesema akiondoka Tip Top ataacha pengo kubwa ambalo haliwezi kuzibika kwa shilingi milioni kumi.
Tunda amekiambia kipindi cha Power Jams kuwa Watanashati bado hawawezi kuleta impact yoyote nchini kutokana na wasanii waliopo na ndo maana wanamhitaji.
Unahisi Tundaman ana thamani ya shilingi milioni 100?

No comments:
Post a Comment