Wasanii wakongwe nchini Soggy Doggy, D-Knob na Bwana Misosi leo wamehudhuria bungeni mjini Dodoma kwa mwaliko rasmi.
Asubuhi ya leo Soggy ameandika kwenye Facebook, “Muda si mrefu mimi,D.Knob na Bwana Misosi tunaingia bungeni leo Dodoma kuona kinachoendelea,ni mualiko.”
Wasanii hao mwezi huu wanatarajia kufanya ziara ya pamoja katika mikoa ya kanda ya ziwa, Ruvuma na Arusha.
Kwa mujibu wa Soggy ambaye pia ni mtangazaji wa Uhuru Fm, ziara hiyo iliyodhaminiwa na PRO-24 imeandaliwa kwaajili ya kuwapa burudani mashabiki wao ambao huwa wanawaona mara chache kutokana na kubanwa na majukumu mengine.
Katika ziara hiyo wasanii hao waliotamba na vibao kama Kibanda cha simu, Nitoke vipi na Sauti ya Gharama wataambana na madansa wao kunogesha show yao.
Huenda wamepitia bungeni kwanza kupata baraka za jengo la bunge.
No comments:
Post a Comment