“Lost my ipad@Airport#off mood,” ni tweet ya Ommy Dimpoz aliyoaindika mchana wa leo. Baada ya kuandika hivyo tuliamua kumpigia simu kujua kama ameibiwa ama imepotea.
Amesema baada ya kushuka Airport ya Dar es Salaam akitokea Mwanza pamoja na MwanaFA, aliiweka kwenye toroli la kusukumia mizigo pamoja na vitu vyake vingine lakini alisahau kuichukua wakati anaondoka.
Hata hivyo pamoja na kuumia kwa kupoteza Ipad hiyo moya aliyoinunua wiki tatu zilizopita, kwa zaidi ya shilingi laki nane, anashukuru kuwa hakuna kitu kibaya ndani yake.
Ameongeza kuwa sana sana, ni video zake tu alizozichukua kwenye show kadhaa alizopiga ndo amezipoteza.
Sikiliza mahojiano mafupi ya simu tuliyofanya naye.

No comments:
Post a Comment