Kama umeshauskia wimbo wa kundi liitwalo ‘Unknown’ linaloundwa na Godzilla, Gosby na Deddy uitwao Sorry, utakuwa umemsikia mtu mwenye flava ya dancehall na reggae mle ndani. Huyu si mwingine ni Deddy.
Sasa hivi jamaa amekuja mwenyewe kuonesha makucha yake. Na ama hakika huyu jamaa amekuja kuikoa dancehall nchini Tanzania. Ladha zake katika dancehall hazina tofauti na wasanii wanaohit sasa hivi nchini Jamaica kama Demarco, Busy Signal na wengine.
Ameachia ngoma iitwayo Bashment time ambayo imefanywa na Phonce wa ‘Feel Good Music.
It’s definitely a massive dancehall issssssh! Check it out
No comments:
Post a Comment