Monday, July 2, 2012

Fid Q – Mi sikufichi, sihitaji urafiki na usupastaa, ukihit ndo unang’aa



Hatimaye video ya ‘Sihitaji Marafiki’ ya Fid Q aliomshirikisha mwanadada Yvonne imetoka leo. Video imefanywa na kampuni ya Showbiz Defined. Na wengi surprise kwenye video hii ni pale palipoandikwa ‘Visualised by Mike T”!

Kwetu sisi hii si video ya kushtusha sana lakini tumefurahishwa na mwanzo mzuri wa Mike T kama director (kama kweli ni yeye ndiye aliyefanya)

Baadhi ya mashairi katika wimbo huu uliofanywa na J-Ryder wa Tongwe Records ni kama haya:

Kupata washkaji ukiwa na pesa ni rahisi
Kupata na hauna kitu jua umefanikiwa kichizi
Mi sikufichi, sihitaji urafiki na usupastaa ukihit ndo unang’aa
Kupishwa kiti kwenye baa, kuwe beat na JR
Siku hizi mabinti wanaonimiss, ndo walionidiss niliposoma nao

Masaa hayarudi nyuma kama muda wa kufuturu
Walioukataa utumwa wameshtuka hawana uhuru
Wanazusha najisikia, so am my own best friend
Naweza nikakata ringi kiasi cha kutopay attention
Lakini sio tajiri wa kuafford kuwa too patient
Sihitaji marafiki labda baadaye akitokea
Aje mmoja wa kuongea naye na mmoja wa kumwongelea

Rafiki wa kweli ni yupi, mkimya ama anaechonga
Yule aliyekupa jina ama ama pengine anayekuponda

No comments:

Post a Comment