Monday, July 9, 2012

Baada ya ajali: Ubongo wa mtoto wa Usher watangazwa kufa



Ubongo wa mtoto wa kambo wa Usher, Kyle mwenye miaka 11, umetangazwa  na madaktari kuwa umekufa.

Hiyo ni baada ya ajali mbaya ya kugongwa na boti (jet ski) iliyotokea juzi kwenye ziwa Lanier jijini Atlanta,GA.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, Kyle Glover mtoto wa mke wa zamani wa Usher, Tameka Foster, hajaonesha dalili yoyote ya ubongo wake kufanya kazi tangu alazwe hospitali.


Mtandao wa TMZ umesema bado hakujachukuliwa uamuzi wowote wa kumwachia ama kumtolea mashine za life support.

TMZ umesema, Usher aliwasili jana hospitali na Tameka hajaondoka hospitali tangu afike.

Kyle aligongwa kichwani na boti hiyo.


No comments:

Post a Comment