Thursday, August 2, 2012

Makala: Makosa yanayofanywa na wasanii wetu wakubwa

Rama Dee

Na Emmanuel Msigwa aka DJ Msigwa: Radio Journalist, Presenter ,Radio DJ & Club DJ, Pride Fm Mtwara

Nimekuwa nikiumia sana kuona wasanii wetu ambao tunawaita wasanii wakubwa, hapa nina imani unanielewa ninaposema “wasanii wakubwa” na nikisema nitaje majina nahisi orodha itakuwa ndefu lakini leo naomba nimtaje mmoja ambaye amekuwa sehemu ya wasanii ambao wanazikosea sana kazi zao hasa video za nyimbo zao na nitaeleza wapi wanakosea,nini wanatakiwa kufanya ili muziki wetu uweze kusonga mbele zaidi ya hapa ulipofikia.

Leo naomba nianze na RAMA DEE, huyu ki ukweli ni mmoja kati ya wasanii wa Tanzania ambao mimi nawaona wana vipaji vya hali ya juu katika aina ya muziki wanaoufanya hasa wanapofanya “rhythm and blues “ yaani r&b nani ambaye hajui sauti nzuri ya jamaa huyu? Nani hajui ngoma kali zilizofanywa na jamaa huyu? Na ni nani pia ambaye haujui ngoma kali alizoshiriki kuzipamba kwa sauti yake tamu? Je unaikumbuka J.O.S.E.P.H ya Prof Jay? Unaikumbuka  ngoma kama RIDHIKA NAMI, SARA,NAJUA na SIYO WAOAJI? Bila shaka hizi si ngoma ngeni masikioni mwako…kifupi jamaa anaweza sana mimi ni mmoja kati ya mashabiki wake!

Kwa sasa jamaa ametoka na ngoma yake mpya inayoitwa KUWA NA SUBIRA ambayo ndani wameshirikishwa rafiki  zake wa kitambo MAPACHA, umewahi kuisikia ngoma hiyo? Kama bado sikiliza ngoma hiyo! Ngoma haina hata mwezi  toka ilipotoka yawezekana wiki mbili tu au tatu toka ilipoachiwa, nakumbuka mimi nilikuwa mmoja kati ya watu waliandika katika “wall” zetu za facebook niliusifia sana wimbo huo na kwangu mimi naona MAPACHA walistahili kuwepo katika wimbo huo.

Licha ya uzuri wa wimbo huo bado napata mashaka ubora wa wimbo huo unaweza kuwa wa muda mrefu? Je ngoma hiyo inaweza kukaa miaka hata kumi (10) ukahit kama ilivyo sasa? La hasha!........sidhani! nakiri tena sidhani! Kwanini? Unaikumbuka  THRILLER ya MICHAEL JACKSON? Unajua ngoma hiyo ilitolewa mwaka gani? Kwa taarifa yako ni kwamba mtayarishaji wa  muziki aitwaye QUINCY JONES alitengeneza ngoma hiyo kupitia album iliyopewa jina hilo mwaka 1982 je ni miaka mingapi sasa? Je umewahi kuona video ya ngoma hiyo? Bila shaka ndiyo!......sasa basi kama haufahamu ni kwamba ubora wa video hiyo ndiyo uliifanya ngoma hiyo kung’ara mpaka sasa kwa nini wasanii wetu hawajifunzi kupitia wao? Je awapati nafasi ya kujifunza kupitia ngoma fulani au ndiyo kusema wanakurupuka?

Je umepata nafasi ya kuangalia video ya wimbo huo wa RAMA DEE wa KUWA NA SUBIRA? Ni video nzuri kwa maana ya rangi,mandhari na uchanganyaji wake wa picha! Vipi kuhusu  wahusika? Vipi kuhusu story board ya wimbo huo? Sijui gharama ya wimbo huo lakini nina imani tena ya dhati kabisa kuwa video hiyo itaishusha sana thamani ya  ngoma hiyo kwa maana ya audio yake, fumba macho wakati unaisikiliza ngoma hiyo halafu wakati huo huo tazama video yake! Je kuna uhalisia wowote? Umewahi kuusikiliza wimbo wa SAME GAL wa R.KELLY & USHER RAYMOND?  Umewahi kuona video yake?

Si huo tu ni nyimbo nyingi sana ambazo naweza kutolea mfano ni kweli, RAMA DEE hajui hicho? Hakuna watu wa kuwashauri wasanii wetu? Au wasanii wenyewe hawataki kuwashirikisha watu wenye upeo wa mambo hayo? Inasikitisha sana! Ki ukweli ngoma nyingi kali za jamaa ambao ni audio zinaangushwa na video zake si pekee yake bali wapo wengi nitawaelezea siku nyingine!

Wakati fulani mwaka 2011 nilipata kushiriki katika mradi mmoja wa waandishi wa habari nchini Ujerumani na kukaa huko kwa muda kuna kitu kimoja upande wa sanaa nilichojifunza kule moja ya vitu hivyo ni namna wanavyosimamia kazi za sanaa na pili ni namna kazi hizo zinavyotoka mathalani album ya msanii au wimbo wa msanii utakaoucheza klabu za disko si ule utakaousikisiliza redioni na kadhalika ni tofauti na utakaouona katika video na wala hautafanana na ule wewe utakaoununua tofauti uanzia katika midundo “beats” baadhi ya mistari “lyrics”  wakati mwingine hutofautiana katika melody zake, hivyo  ndivyo wenzetu wanavyofanya kikubwa zaidi ni kwamba nyimbo zao ubebwa na ubora wa video zake na ndiyo maana wasanii wengi wa Marekani utoa kwanza video za nyimbo zao kabla hajasambaza audio zao.

Tungependa kuona video za wasanii wetu zibebe pia theme ya wimbo husika, kama mtu akizungumzia suala la kumsifia mpenzi/mke wake kwa mapishi mazuri basi tuone kipande cha muhusika akipika na si kuona anachota maji au kuona tabasamu lake!.............ndugu zangu, rafiki zangu wasanii badilikeni hili kazi zenu zidumu miaka hata 30 zaidi ni kuboresha video za NYIMBO ZENU!

Naomba kuwasilisha

No comments:

Post a Comment