Justin Bieber alilazimika kuendesha gari lake kwa speed ya kufa mtu kiasi cha kumweka katika hatari ya kupata ajali ama kwenda jela kwa kosa la kuendesha mwendo kasi.
Diwani wa jiji Los Angeles Dennis Zine aliyewahi kuwa polisi wa barabarani kwa miaka 18, alimshuhudia kwa macho Justin aliyekuwa kwenye gari lake aina ya Fisker Karma akipita kwa speed inayozidi 100 mph.
Zine ameuambia mtandao wa TMZ kuwa Bieber alikuwa akijaribu kuwakwepa mapaparazzi waliokuwa wakimfuata kwa nyuma.
Zine anasema, “ Bieber alikuwa anaendesha kama mwehu. Alikuwa akiingia na kutoka kwenye traffic. Hakukuwa na nafasi za kutoka katikati ya magari wakati alipokuwa akihama upande na upande.”
Aliendelea kusema "Kama ningekuwa kwenye patrol, ningemkamata kwa kuendesha mwendo wa kizembe. Nilikuwa naendesha kwa speed ya 60 na akanipita kama vile alikuwa kwenye roketi. Alikuwa mwehu.”
Zine pia alisema mapaparazzi hao walikuwa wajinga kuendesha bega kwa bega kwenye freeway na kuhatarisha maisha yake.
Baada ya Justin kusimama paps kama wawili walizonga gari yake.
Hata hivyo meneja wa Bieber Scooter Braun, ameiambia TMZ: "Ni vile tu diwani huyo anatafuta headline."
Braun amesema Justin alionekana kuwa alikuwa akiendesha kwa speed ya 80 mph na alikuwa akifukuzwa na mapaparazzi. Braun aliongeza kuwa baada ya kuruhusiwa makanjanja hao waliendelea kumfuata na ndipo alipoamua kupiga 911.
Baada ya Bieber kupiga 911, polisi waliimfuata na kumsimamisha tena huku mapaparazzi wakiendelea kumfuata nyuma. Mtandao huo umesema polisi waliwaonya mapaparazzi kujiheshimu na wote waliambiwa wasambae.

No comments:
Post a Comment