Friday, August 3, 2012

The Music Postmortem: Izzo B Ft. Belle 9 – Utarudishwa




Wiki hii Izzo B ameachia ngoma yake mpya iitwayo Utarudishwa, aliyomshirikisha Belle 9. Ngoma imefanywa na maproducer wawili. Beat imetengenezwa na the rapper turned producer One the Incredible na baadaye Izzo akaenda hadi Morogoro kwenye studio za Dirty Mode Records ambako producer Tris alimalizia kazi iliyosalia. Panel ya TMP inauchanachana wimbo huo kama ifuatavyo:

Josefly

Kwanza kabisa niseme tu nilikua surprised kidogo niliposikia beat ya hii ngoma ameinyonga One the incredible, big up kwake kwa kuwa multi talented, japo naona inaendana na ile ya IZZO B ft. Suma lee, IZZO BUSINESS ,au hizi ndo beat za IZZO B.! Ila ni beat nzuri ya Hip Hop.
Sasa nazama deep kwenye ngoma yenyewe na nitaegemea kwenye mashairi na utunzi wa hii ngoma, kwa ufupi tu hii ngoma nina mengi ya kuielezea kwa kuichalenge na kuisifia pia ila nitayafupisha. Naanza na challenge ili zieleweke mapema.

Wimbo ni wa kawaida, kama mtu anamjua Izzo B, sio mbaya na wala siwezi kusema ni wimbo mkali, labda tu niseme wimbo ni mzuri, hapo naamini nimeeleweka, sio mkali ila sio mbaya pia.

Huu ni wimbo wa hip hop ambao umeandikwa kama ‘free of style’, kwa wafuatiliaji wa hip hop watakua wamenielewa zaidi ya ile maana ya freestyle iliyozoeleka. Kiitikio cha wimbo kinaashiria tu kumuonya Izzo kwa anachokisema kuwa kinaweza kupelekea yeye kurudishwa kwao Mbeya. Na hapo ndo hiyo free of style inanifanya nisikilize ili nijue kasema nini Izzo hadi his big boy Belle anamtahadharisha kua atarudishwa kwao Mbeya baada tu ya verse ya kwanza, nilijua atasema chochote coz chorus haimbani ila nahisi itakua ni mambo fulani mazito hata kama ni majigambo.

Daah, bahati mbaya kiukweli Izzo hakuweza kwa asilimia 100 kunipa kile nilichotegemea, japo sijui angeimba nini kwa sababu the song is free of style kwa hiyo nitahukumu nilichosikia tu, mi naona kwa hii chorus nadhani ameitendea haki kwa asilimia 70 hivi kiuandishi, ni asilimia kubwa labda ndo sababu wengi hawatashitukia, ila sikiliza tena na tena na nifatilie ninachosema pia. Verse ya kwanza aliianza vizuri ila mi naona kabisa ikiingia chorus labda neno analomaliza nalo ndo linaipa push kidogo chorus kuanza hivo. Ila duh..bado kidogo.

Chorus ya maneno mawili naona kama imezidi kidogo uzito kile kilichoimbwa, jaribu kusikiliza kwa makini jinsi Belle 9 anavyomtahadharisha, tengeneza picha ya hii tahadhari na mashairi anayoingia nayo Izzo B, ni majigambo ya kawaida tu ambayo yangekaa kwenye chorus yoyote ya majigambo, haya maneno mawili ya kwenye chorus ni ya kawaida sana ila yanatoa picha nzito saaana ya kinachoimbwa so mashairi ya Izzo kama kidogo yamezidiwa uzito kwa mtazamo wangu. Na hapa napapigia mstari.

Pia kuna mstari naona kama Izzo aliamua tu kumtaja Chidi, “natubu kama Chid japo sitokei Ilala” kweli kuna uhusiano kati ya kutubu na Chidi kwa ngoma yake ya NATUBU..lakini mi sioni mahusiano yanayoleta maana kati ya kutubu na kutokea Ilala. Inamaana wanaotubu sana ni wa Ilala? Najua imezoeleka sana kutumia aina hii ya uandishi ila hapa pande mbili hazina mahusiano, hasa kutubu na kutokea ilala, imejazilisha tu line!

Mbali na hayo, kiukweli sijasikia tofauti sana kati ya hii ngoma ya Utarudishwa na Ile Izzo Business, chukua hizi ngoma mbili zisikilize then utaona ni kama kapita njia moja ila kabadili tu mavazi, ni mulemule kwa msemo wa kisasa. Mashairi yamebadilika kidogo, lakini hii ni kama part 2 hivi kwa maudhui, na nadhani haya mashairi pia yanakaa kwenye ile chorus ya IZZO BUSINESS aliyofanya Suma Lee zaidi ya huku kwenye hii chorus ya Belle 9 kimaudhui.

Tukiachana na hizo changamoto, Izzo B amebarikiwa kughani kwa ladha fulani nzuri kusikiliza katika kila neno analotamka kwa Kiswahili au kiingereza, pia kuna maneno mazuri na punch line au ‘mistari konde’ mingi kwenye hii ngoma, na maneno yanayojenga picha flani nzuri sana.
Mashairi kama mashairi tu yako poa. Stile ya kuwakilisha mashairi iko poa na imeendana na beat. Ni hayo tu.

Kinye

Karibu Izzo kwenye uwanja wetu.

Utarudishwa Mbeya”…nadhani ingekuwa hivyo, si kwa ubaya lakini ni kama haijitoshelezi kuitwa utarudishwa, ni kama kinywa kinadai maneno zaidi kuridhika.

“One”…mkali wa michano ambaye haoni future yake kutakata nje ya muziki (nilibahatika kumsikia akijinadi hivyo siku moja). Mdundo huu umenifanya nianze kuamini kuwa akijitahidi basi kweli ndoto yake ya kuwa bonge la mundaaji yaweza timia kwani huu umekuwa mwanzo mzuri huku nikiwa naamini kuwa kitaalamu anahitaji mawili matatu kuweza kuimarika zaidi.

“Belle”…BLOG hii imemtunuku taji la ukali wa chorus kitu ambacho kilikuwa kigumu kupinga kwakuwa ni kweli tupu. Nimefurahi hajakomaa kama anavyokomalia viitikio vingine, hii imetoa ladha mpya na tamu japo mpaka sasa natamani sauti ya Izzo isingekuwa inasikika kwenye kiitikio ili kuleta maana zaidi!! Kwa maoni yangu angeachwa Belle kuamua namna ya kukamilisha maneno yote ya chorus kwa namna yake.

“Izzo”…toleo lako lingine hili ambalo si baya kiukweli japo pia si zuri kupita matoleo yako yote mengine. Siku zote nimekuwa nikipenda mawazo yako ya kiuandishi na mtindo wako ambao kwa kiasi una upekee…hongera kwa hili.
“Tris ”…bado sina mengi juu yako kwakuwa wafanya vizuri japo si kupita wote, pokea hizo pongezi. Kwenye wimbo huu na nyingine zoote kila neno litamkwalo naamini haki yake ni kusikika kwa ufasaha, kama hili tunakubaliana basi niseme ulipitiwa kidogo kuruhusu sisi kutosikia baadhi ya maneno kwenye wimbo huu, nazungumzia kwenye kiitikio ambapo kuna maneno sijayasikia yanatamkwa kumaanisha nini, na shida imekuja baada ya wewe “kubend pitch” ya maneno hayo…kiukweli mimi sikuona umuhimu wake pale.

Amani Joakim

Ni Ngoma nzuri sana,nafikiri hakuna muziki mbaya hata siku moja.. Hata Hivyo, nimemskia Izzo B akiimba nyimbo kama hii zaidi ya mara tatu,sidhani mimi kama mskizaji ningependa kusikia kitu hicho hicho hata kama ni kizuri kutoka kwa mtu mmoja.

Ana uwezo wa kubadilika na nina hakika ana vitu vingine lakini akifuta ile formula ya "FOLLOW THE SUCCESS TREND UNTILL IT BREAKS" nafikiri inaweza kumfikisha pabaya. Ukifuata hii formula unaeeza ukakuta mashabiki wako baadhi wanakufuta kwenye list zao halafu kurudi itakugharimu nguvu kama vile unaanza Muziki.

Belle 9 kama kawaida amefanya vizuri kwenye sauti za Chorus. Kwenye swala la Mdundo..Ni Beat nzuri sana hasa ikiwa imetengenezwa na mtu aliezoeleka kama Artist. Mdundo una hadhi zote za hip hop.
Nafikiri mdundo huo una purpose ya watu kusikiza kinachosemwa zaidi hivyo mtu halisi aliyetakiwa kukaa ni yule mwenye maneno ya msingi lakini yasiyochosha pia..kama ONe The Incredible Vile..

Asilimia 90 ya wasanii Bongo na hata America wanahitaji beat nzito na yenye vionjo vingi ili kuweka mzani pale ambapo mashairi yake yanapokua dhaifu kidogo,ndio maana ni mara chache utamskia ama usimskie kabisa Nas/common kwa beats za Timbaland ama Polow Da Don ama Jim Jonsin (wote wamefanya nao lakini sio watu wao wa mara zote) ni kutokana uzito wa mashairi yao unaitaji kitu simple kama Mdundo huu, ambacho producers hao ambao ni Heavy Hitters sio mikato yao.

Ushauri wangu ni kwamba Izzo afanye mpango wa kubadili hii formula ya Political Theme ambayo ameifanya mara kadhaa tayari kabla haijamuharibia.
Lakini pia inaweza kuwa ni formula inayomfanya awe Izzo B. Kwa kuwa yeye ni msomi nafikiri atafanya utafiti kabla ya kuchukua hatua yoyote ya mabadiliko. Pia awe mwangalifu na aina ya midundo anayochagua mingine ni hatari kwa afya ya career yake. N:B. Mawazo haya ni ya kwangu binafsi, nina haki ya kueleza na sio shuruti kuyafuata.

J-Ryder

Kwa Beat Making, One Incredible amejitahidi, compared na kipinde cha nyuma, back then.

Sample ingekaa poa ingeongezwa Stereo Widening, ipo sana Mono.
Kwa Chorus, sijapenda pale Belle 9 anaposema "Izzo, izzo", kama wange umiza kichwa zaidi, ila kipande cha pili "utarudishwa Mbeya" naona imekaa sawa.

Upande wa vocals, ukisikiliza vizuri unaweza hisi kuwa imekuwa recorded pembeni tu ya computer equipments, na kama ni kwenye booth ama vocal room, basi Acoustic Treatment yake bado sio nzuri.

Kwenye Bass, ingewekwa Bass Amps ili kuongeza Volume yake...na pia ku-separate Bass na Kick by cutting unwanted frequencies.

Bila shaka ngoma imekaa okay, mixing tu hapa na pale, automations kidogo..itakaa sawa.


No comments:

Post a Comment