Friday, July 6, 2012

Rihanna kuipeleka kortini kampuni ya uhasibu kwa kumuibia




Rihanna anaipeleka mahakamani kampuni yake ya zamani ya uhasibu kwa shutuma za upotevu wa mamilioni ya dola zilizokusanywa kwenye show zake nne za kitaifa na kimataifa.

Mrembo huyo ameandikisha kesi hiyo kwa jina lake halisi Robyn Fenty kwenye mahakama ya Manhattan kuishtaki kampuni ya uhasibu yenye makazi yake New Yorkya Berdon LLP kwa kesi ya madai.

Kwa mujibu wa ripoti ya Associated Press, kampuni hiyo imetia kibindoni mamilioni ya dola katika kipindi cha miaka mitano.

Kesi hiyo inadai kuwa kampuni hiyo ilifanikisha kutia mfukoni karibu asilimia 22 ya mapato na kumpa Rihanna asilimia 6 tu.

Baada ya kulitimua kampuni hilo September 2010, timu ya Rihanna iligundua ongezeko kubwa la faida kwenye ziara zilizofuatia.

Rihanna aliliajiri kampuni hilo kipindi akiwa na miama 16 wakati ndo anaanza muziki.

No comments:

Post a Comment