Sunday, July 1, 2012

Ni nani huyu aliyempagawisha Diva hivi?



Okay, umpende usimpende, Loveness aka Diva ni mtangazaji anayezungumzwa zaidi nchini. Ukianzia kwenye kipindi chake mpaka maisha ya kawaida, ni full of drama.

Mwezi uliopita alitoa ngoma yake ‘Piga Simu’ akiwa na Diamond na imepata promo ya nguvu husasan kwenye kituo anachofanyia kazi, Clouds Fm, si unajua mcheza kwao hutuzwa!

Well, kisa cha wimbo huo ni kwamba jamaa yake ni mtu wa mishemishe sana kiasi ambacho anakuwa hana muda wa kutulia sehemu naye na kuenjoy mahaba yao. Inaonekana ni mtu fulani hivi mambo safi sababu jamaa ni mzee wa kukwea pipa kwa sana.

So ndo Diva akaamua kuandika wimbo huo kumtaka walau ampigie simu ili japo asikie tu sauti yake. Tangu atoe wimbo huo, kwenye page yake ya Twitter pamoja na kuandika mambo mengine, amekuwa akiandika ujumbe mwingi kuonesha ni kiasi gani anamzimia mchizi huyo.

Na pia kwa sasa amesharekodi wimbo mwingine uitwao ‘Mgonjwa kwa raha zako’ maalum kwaajili ya jamaa huyu huyu. So who the hell is this guy? Kampa nini mtoto wa watu mbona kadata hivi?

“I love u so much, God knows how much I do love u, its only u , tried to think of u in every step I take, My heart stuck with only u,” aliandika wiki hii.
“Hope one day u will understand how much I truly love u, whatever u do jus kno that I love you,”

“Been in love with u completely. I love ma baby .....so in love with him , I lovE ma baby ‪#singing.”

“Mwinginewe achomozi nakupenda peke yako , Daima nitakuenzi silitupi Pendo lako. Naingia simanzi kukukosa siwezi...Wallah sijitambui mgonjwa kwa raha zako ......

Nakesha macho kwa kutia toba ...... Kofi zito limenizaba kisa mahaba ... Ananionea eeh???

Nakonda na kukosa haiba ..... Kisa kupenda, macho yameziba kisa mahaba , ..... ♥♥

Na ili kuonesha kuwa baadhi ya maneno hayo yatasikika kwenye wimbo wake aliandika, “Lile busu Pembeni ya bahari , na ule upepo mwanana nakupenda sina hali .... Finishing mgonjwa kwa raha zako at Fishcrab.”

Anyway shout outs to the dude! He is good.

No comments:

Post a Comment