Wednesday, July 4, 2012

Wanamuziki watatu wa Kenya wakamatwa kwa kuimba nyimbo za chuki




Wanamuziki maarufu nchini Kenya wamekamatwa kwa tuhuma za kueneza ujumbe wa chuki kupitia nyimbo zao.

Nyimbo hizo zilizoimbwa kwa lugha ya Kikuyu zinamuunga mkono naibu waziri mkuu wa Kenya Uhuru Kenyatta ambaye ni mkikuyu.

Madai hayo yametolewa na tume ya mshikamano wa kitaifa (NCIC), iliyoundwa baada ya kutokea vurugu za baada ya uchaguzi nchini humo mwaka 2008.

Hata hivyo waziri Kenyatta amesema hana uhusiano na wanamuziki hao wanaopinga madai hayo.

Nyimbo hizo za Kamande Wa Kioi, Muigai Wa Njoroge na John DeMathew zinadaiwa kuchochea vurugu kati ya watu wa kabila Kikuyu na wajaluoa ambao wanamuunga mkono waziri mkuu Raila Odinga.

Wote Uhuru na Odinga wanagombea urais katika uchaguzi ujao.

Kama wakipatikana na hatia, wanamuziki hao ambao wapo nje kwa dhamana, watakabiliwa na kifungo cha miaka mitatu jela ama faini ya karibu shilingi million 20 za Tanzania.

No comments:

Post a Comment