Friday, July 6, 2012

The Music Postmortem: Party Zone ya AY Ft. Marco Chali




AY aliamua kuachia video ya wimbo huu kwanza. Video ilifanyika Afrika Kusini na kumgharimu pesa ndefu. Baada ya siku kadhaa ndo akaachia audio yake. Leo hii panel ya TMP inaichambua Party Zone kama ifuatavyo.


Joseph ‘Josefly’ Muhozi

Kama kawaida mimi nitaegemea zaidi katika upande wa mashairi kwa asilimia kubwa. Lakini nianze tu kwa kugusia kiujumla...wimbo ni mzuri kwa upande wa IDEA, ni idea flani unique kwa nyimbo ambazo zimeshaimbwa na wasanii wa hapa Tanzania. AY ni kama vile ameamua kuyapotezea maumivu ya mapenzi na kufungua ukanda wa ‘shangwe’ kivyake badala ya kuendelea kulialia na maumivu ya mapenzi kwa mtu ambae ali-mteat vibaya.
Wimbo umepangiliwa vizuri, hasa mwanzo kwenye kibwagizo ambacho kinaleta ladha flani kwa maneno yanayofanana fanana yakitamkwa yanaleta ladha nzuri na mtu anaweza akajisikia kuyarudiadia...

          Skiza hii ndo ‘ fact usiact’  like you don’t know
          The way you treated me umeshanipa somo

Chorus yenye msitari mmoja tu, iko poa kwa sababu kibwagizo kinajieleza na verse ya kwanza inayotoa maana halisi ya kwa nini ‘party zone’
Huu wimbo uta-Hit lakini naamini itatokana na  sababu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na style ya kuimba na kurap, mdundo unaohamasisha, and other factors..lakini sio uzuri wa uandishi wa mashairi. Hapa namaanisha kua katika uandishi wa mashairi kwa kweli mtunzi/watunzi hawaku-explore uwezo wao wote ( kutumia uwezo wao kwa kiwango cha juu kuandika mashairi, kwa sababu wote tunafahamu uwezo mkubwa wa AY katika medani ya muziki), na hii ndio sababu sishawishiki kukubali kua ndipo alipoishia katika utunzi wa haya mashairi.


Labda aliamua kuandika mashairi simple!! sina uhakika, to be honest mashairi ni mepesi sana tu. Inawezekana pia sijaeleweka naposema mashairi ni mepesi, lakini wepesi huu wa mashairi utaupata kwa kulinganisha ukubwa wa AY kimuziki na usanii wa uwandishi uliotumika kufikisha hii IDEA nzuri ya wimbo. I expected something bigger......

Wepesi huu wa mashairi unaweza usionekane moja kwa moja kwa sababu umefichwa zaidi na style ya kuimba na kurap iliyotumika, ambayo imekaa poa, na mdundo unaohamasisha. Kwa hiyo kama unataka twende sawa hebu yatoe mashairi haya kwenye instrumental, na hiyo melody..kama umevitenga sasa unaweza kukubaliana na mimi kwa sababu muziki sio melody tu kama wengi tunavyopeana moyo siku hizi hapa bongo, mashairi mazuri yanaongeza life span ya wimbo kwa sisi wasikilizaji, kwa jinsi ujumbe ulivyofikishwa. Ubunifu usionekane tu kwenye melodies na instrumental (mdundo) ila inatakiwa uende hadi kwenye uandishi, ili kila kimajawapo kikitengwa kisimame kwa upande wake (beat kali, melodies, rap style, na mashairi makali).

Kwa kuongezea tu, wimbo umebebwa zaidi na ki-SWANGLISH  katika swala zima la uandishi ambapo hii imefunika funika mabonde ya wepesi wa mashairi, maneno ya KISWANGLISH sio kama yameongeza uzito wa mashairi bali yameleta fleva ambayo haichoshi, japo siamini kabisa kua maneno ya kiingereza yana ladha nzuri zaidi ya maneno ya Kiswahili.

Unaweza kusema labda ni kwa sababu ni wimbo wa kuimba ndo sababu mashairi yakawa hivi, lakini hata alipoingia kurap, bado kiswanglish ndicho kilichotawala sehemu kubwa na kuleta ladha tofauti kama nilivyosema.
Lakini mbali na mashairi, AY amefanya style nzuri sana hasa ya kurap na melody, na beat inaendana kabisa na wimbo huu ‘party zone’  ambavyo kweli vinahamasisha ku-party. Nategemea ngoma zinazokuja atakazofanya MJ records zitabalance pia katika uandishi....


Wynjone Kinye

Niseme wazi kuwa assignment hii haikuwa nyepesi hata kidogo, na wala haikustahili kuwa nyepesi “kucritic” mtu mwenye hits za kutosha na mwenye mafanikio makubwa kimuziki bila kusahau heshima kuu ndani na nje ya nchi.

Sikutaka kujitesa sana…nikaamua kujikusanyia watu “laymen” ili waseme kitu juu ya wimbo huu. Kila niliyemsikilizisha aliufurahia na mwisho nikimuuliza unahusu nini anasita kidogo na kusema “huu ni wimbo wa party….sikulaumu as wimbo wenyewe unaitwa “Party is On/Party Zone” japo unazungumzia kutendwa visivyo penzini na kupotezea stress kwa kula bata.

Sikupata msaada mkubwa sana toka kwa watu kiukweli, wanachojua wao ni kuwa mzee wa commercial karudi tena na kama kawaida wamempokea…ikabidi nikae mwenyewe na kuusikiliza tena na tena huku nikinote viwili vitatu kama ifuatavyo.

Miongoni mwa Elements muhimu za wimbo ni “title”…ni kitu msikilizaji atakumbuka na kutaja pindi auhitajipo wimbo (kama ameupenda lakini). Kitu cha kwanza atakachosikiliza mtu ukiacha intro ni mistari ya kwanza (maneno na namna yalivyoimbwa). So let me look at Ay’s.
“uliniona sifai, ukaniacha ukaenda mbali, dunia imekuonyesha, sasa unataka urudi…” nafurahi kwakuwa mpaka sasa tumeshajua wimbo unahusu nini (kimistari) japo . most people at some point of their lives have thought the same or similar words kitu ambacho si chema sana kwenye kazi ya sanaa…lakini pia hakika bado kujua nini Ay anataka kufanya (kiuimbaji).

Nikiri kuwa wimbo huu una melodies nzuri na nyepesi, watu wataushika na kuucheza club ila honestly its not a “waoh” song…kiroho safi kabisa sababu iko wazi kuwa Ay si muimbaji kiviile, heshima yake inabaki kwenye upande mwingine (michano). Aimbapo basi hudondokea kwenye kundi la wakina puff dady ambao “si wakali lakini wanakata”…

Sijui ni sikio langu ama, kwakuwa hii ni nafasi nimepata basi niitumie tu…mara nyingi huwa Napata ugumu kusikia Ay anatamka nini, na hii si kwa wimbo huu tu bali nyingi za huyu bwana, sijui anaenda haraka sana ama anamung’unya sana???

Intro nzuri toka kwa Marco Chali na maneno machache na rahisi kushika kwenye kiitikio…kwenye production nisitie neno mie…. Musically speaking, it is a fair track…keep up the good work.

Fredrick 'Mshale' Max

Ay kwa Mara nyingine tena....Safari hii na club banger Partyzone..nyimbo hii ni nzuri kiasi na Ay pamoja na Marco Chali wanastahili Pongezi kwa kuchuckua risk...na style hii ya muziki. Wote tunamjua Ay Kama mzee wa commercial hivyo hatukushangaa sana kwa yeye kutoka na style tofauti, japokuwa mashairi ya wimbo huu yako weak. Wahusika wanaeza kusamehewa kutokana na nyimbo yenyewe kuwa ya ku party zaidi, hivyo basi mtu atazingatia zaidi midundo na vionjo.

Ay is dancing his troubles away baada ya kuachana na mpenzi wake. Beat wamejitahidi japo wangeweza kufanya vizuri zaidi, they have taken us to the dance floor, halafu wakatuacha katikati, ingekuwa poa kama tunge get loose kabisa.

Anyway Party Zone is a nice tune...nothing spectacular but good....naipatia nyota 3 Kati ya 5....haya bongo fleva inaenda dance/house route..from utanikumbuka by suma lee na sasa party zone ya Ay...kudos...

J-Ryder

Video bila shaka imefunika audio..first time nilipoisikia..video yake ndo ilinifanya niicheki tena na tena. Audio wise kwangu naona ni poa ikichezwa club sana kuliko on radio stations.

Kwenye audio yenyewe sasa...sijajua vision yao ya beat ilikuwa upande gani exactly..kwasababu genre yake imeandikwa "Bongo Flava"!! na sio Electro Dance n.k..na kwa genre ya electro dance, basically the kick na bass (bottom end) ndio they have carry the song..

Tempo yake ni around 125 bpm, naona ingekua poa iende mpaka 128. Arrangement ya beat, ipo okay ila inahitaji more work on the breakdown. Breakdown ni ile build up towards the main part ya song...

The vocals were tracked well from my prespective, zimetoka freshiii..ambacho nimeona sio ni pale anaposema "pa-pa-pa-pa-party zone" ...izo "pa" angezi cut on the lower frequencies.

Kingine ni kwamba delay aliyotumia ipo sana centre (mid part), ni poa sana ikiwa "ping-pong" ambayo inakuwa kama automation Left to Right, ili delay feedback iweze kuwa more wide...another issue ni kwamba the "kick" ain't having enough of that "ENERGY" feel...
Also the "Pitch-rise" effect haipo poa sana, too simple...

"sikia hii ndo fact, usi act like u dont know..the way you treated me ulisha nipa somo"...ahhh kumbe pale kwenye somo ni "so more"..party zone pia unaweza dhani ni "party is on". Ila kazi waliyo-ifanya ni nzuri.


  



No comments:

Post a Comment