Monday, May 7, 2012

Maproducer mpo? STL anatafuta beats, changamkeni!



















Baada ya Lookie Lookie, Hula Hoop aliyomshirikisha Mohombi na Habahaba zilizokuwa na mahadhi ya pop/dance sasa Stella Mwangi aka STL anataka kurudi kule tunakomkubali, kwenye hiphop. 

Ngoma kama The Dreamer na She got it zinauelezea vema uwezo wake katika kuchana.
 
Kipindi hiki STL amekuja na good news kwa maproducer hasa wanaochupikia. 
 
Guys STL anahitaji mdundo?


“If u got any hot Dancehall, Crunk, Afrobeat, HipHop beats, send to beats4stl@gmail.com #TheGurlGetsBussyyy”  ameandika.


Changamkieni mchongo huo. Mara nyingi wasanii wakubwa kama hao wana nafasi kubwa ya kuvitangaza vipaji vya maproducer wakali wasiojulikana.


No comments:

Post a Comment