Showing posts with label EAST AFRICA SHOWBIZ STORIES. Show all posts
Showing posts with label EAST AFRICA SHOWBIZ STORIES. Show all posts

Saturday, August 18, 2012

Keko aongea na Leotainment, kuwasili Mwanza kesho saa 2 asubuhi



Rapper wa kike kutoka nchini Uganda Keko amesema anatarajia kuwasili jijini Mwanza kesho saa mbili asubuhi.

Keko ambaye hii ni mara ya kwanza kuja Tanzania, ataperform kwenye hoteli ya Star Max.

Amesema pamoja na kuja Mwanza tayari yupo kwenye mazungumzo na MwanaFA kwaajili ya kufanya ngoma pamoja. ‘I am big fan of Mwana FA we are actually working out something as we speak . I am looking forward and hopefully bumping to Fid Q when I am in Mwanza, ” amesema.

Ameongeza kuwa kama kuna promoter yeyote wa Dar es Salaam ambaye angependa kufanya show naye nafasi ipo wazi.

Sikiliza interview yote hapa

Picha ya boksa ya Afande Sele yafananishwa na Bebe Cool, Bebe awaka!



Hii story inachekesha sana. Kuna madj nchini Uganda wameichukua ile picha maarufu ya Afande Sele aliyoteremsha suruali na kubaki na boxer kwenye stage na kudai kuwa huyo ni Bebe Cool.

Baada ya kuona hivyo Bebe Cool amekasirika kiasi cha leo kuandika kwenye page yake ya Facebook na kufafanua kwa mashabiki wake.

"hahahaha, I pity two silly fools, one works in Club Rouge as a cleaner by the names Onyango Gareth the other is a wanabe DJ mbu DJ Jojo Mimz as short as a shoe. They post a fake pic of some up-coming tz artist called Afande Saly performing at a Tigo promo in TZ to counter attack the A and B story that I posted. Only they forgot that in UG thez no tigo and Bebe is a lot mo hairy and has mob side bans. sori ma fans aint drug addicts like A and B fans. ma fans can see"

Tumeongea  na Afande Sele kuhusiana na taarifa hiyo na kudai kuwa haifahamu na kusema kuwa anamuona Bebe Cool kama underground ndio maana hajawahi kupata show Tanzania.

Afande amesema msanii anayemkubali nchini Uganda ni Chameleone na Bebe Cool anasema ni mshamba tu.

Msikilize Afande hapa.

Friday, August 17, 2012

Miss Karun wa Camp Mulla bado bikira!!



Wanaume wa Kenya wanaommendea first lady wa Camp Mulla, Miss Karun, inabidi wajiandae kukutana na mama yake ambaye ni mkali zaidi ya mbogo!

Inadaiwa kuwa japo Miss Karun ameshauvuka umri wa hatari unaoweza kumpeleka kidume jela kama akila 'tunda' lake, mama yake hamruhusu kuwa na mpenzi.

Mama yake ni wale akina mama ‘wakoloni’ na matajiri ambaye hawezi kumruhusu mwanae huyo mrembo aende kwenye concert na kukosa masomo, hata kama inalipa kiasi gani!


Anasoma kwenye shule yenye gharama nchini Kenya iitwayo Braeburn.

Inadaiwa kuwa mama yake humchagulia hadi nguo za kuvaa. Siku ya fainali ya Tusker Project Fame mwezi uliopita ambapo Camp Mulla waliperform alivaa nguo ambazo mama yake hakuzikubali.

Inasemekana kuwa aliporudi nyumbani alichezea kichapo cha paka mwizi na kuambiwa kuwa siku nyingine akiperform anatakiwa aufunike mwili wake kwa kuvaa soksi ndefu ama tight.

Thursday, August 16, 2012

Keko kupiga show jijini Mwanza weekend hii



Rapper wa kike wa nchini Uganda Keko anatarajiwa kupiga show weekend hii jijini Mwanza.

Taarifa hiyo ameitoa mwenyewe kupitia Twitter.

“TANZANIA ARE YOU READY!!! #KEKONIANS IN MWANZA #MAKEYOUDANCE COMING TO YOU THIS WEEKEND tell every & anyone KEKO Coming!!”

Hata hivyo mpaka sasa haijawa wazi ni nani anayempeleka jijini humo ama show itafanyika wapi kwakuwa hakuna matangazo yaliyotolewa.

Wednesday, August 15, 2012

Prezzo: Mungu alikuwa na sababu yake kunifanya niwe namba 2


Mshindi wa pili wa shindano la Big Brother Africa Stargame, Jackson Makini aka Prezzo amesema Mungu alikuwa na sababu yake kumfanya akamate nafasi ya pili.

Amesema anaamini kuwa kwa nafasi hiyo kuna mengi mema yapo njiani yanakuja kwaajili yake.

Akiongea na kipindi cha Amplifaya cha Clouds Fm, Prezzo amechukua muda huo kuzungumzia pia taarifa ya gazeti la Daily Post la Kenya lililodai kuwa atakuwa akilipwa dola 720,000 kwa mwaka kama balozi wa One Campaign.

Amesema ameshangaa kuona habari hiyo na kudai kuwa anatamani ingekuwa kweli kwakuwa hakuna kitu kama hicho.

Msikilize zaidi hapa kwenye interview hiyo.

Picha zaidi za party ya kumkaribisha nyumbani Prezzo

Mapacha wa BBA
Mwendo wa Ciroc tu!
Hotties
Prezzo na waziri  Eugine Wamarwa
Prezzo na Alex wakionesha kuwa hakuna tena beef kati yao




Popping Bottles











Monday, August 13, 2012

Video: First Lady wa Camp Mulla (Karun) akionesha uwezo wake


Wakati kundi la Camp Mulla la nchini Kenya likiwa limeshajipatia umaarufu mkubwa barani Africa kwa nyimbo zake kali na video za maana, muda umefika wa members wa kundi hilo kuanza kuonesha uwezo wa kila mmoja. Miss Karun ambaye katika nyimbo nyingi za kundi hilo amekuwa akisikika kwenye chorus na bridge zaidi, ametoa video hii kuonesha uwezo wake awapo mwenyewe. Ama hakika mtoto huyu mrembo Mungu kamjaalia kila kitu. Ukiangalia video hii, ni rahisi kupata jibu kuwa hata kama akisimama mwenyewe, Miss Karun ni star we peke yake. 



Ana kipaji na muonekano wa kuvutia kuuzika kimataifa. Record label yoyote ile itakayoona video hii haitasita kumsainisha yeye kama yeye. Enjoy video hii huku ukiangalia sura nzuri ya mtoto huyu mrembo mwenye ngozi halisi ya Kiafrika. Mashalaah!


Picha: Party ya kumkaribisha Prezzo, Carnivore, Nairobi

Malonza, Prezzo na Alex
Nipeni tano
Prezzo na mashabiki


Poppin Bottles
Salute
Prezzo na hotties wa Nai!

Friday, August 10, 2012

Exclusive: Prezzo atakuwa akipokea bilioni 1.4 kwa mwaka!!!



Gazeti la DAILY POST limeandika kuwa mshahara atakaokuwa anapokea Prezzo ni dola 720,000 kwa mwaka akiwa balozi wa One Campaign.

Fedha hizo ni sawa na shilingi bilioni 1,  milioni 137 na ushee za Tanzania!

Kwa mshahara huo Prezzo atakuwa akilipwa zaidi kuliko hata viongozi wakubwa   Kenya.

Mshahara wa rais Mwai Kibaki ni shilingi za Kenya milioni 3.2 sawa na milioni 57 za Tanzania na waziri mkuu Raila Odinga akipokea milioni 2.4 za Kenya huku Uhuru Kenyatta akipokea kama milioni 1.5 kwa mwezi.

Hii ndo payslip ya Prezzo:

Mshahara kwa mwezi :      $40,000                    (TSH 63,200,000)
Posho ya nyumba :           $5400                       (TSH 8,532,000)
Posho ya usafiri :             $6600                      (TSH 10,428,000)
Kuburudika:                     $5000                        (TSH 7,900,000)
Matibabu:                       $10,000                     (TSH 15.800,000)

Vingine:  Passport ya kidiplomasia na walinzi wawili.

Pamoja na hivyo bado kuna marupurupu mengine yanayoufanya mshahara wake kwa mwezi kufikia karibu 189,734,400!!!

Thursday, August 9, 2012

Picha: Prezzo na bodyguard kama president vile!!


Umaarufu wa Prezzo nchini Kenya na hata Afrika kwa ujumla umeongezeka maradufu.

Awali alikuwa anajulikana kwenye jamii ya vijana zaidi wanaofuatilia muziki wa hip hop lakini miezi mitatu aliyoitumia nchini Afrika Kusini kwenye jumba la Big Brother Africa, imemboost zaidi na hiki ndio kipindi ambacho atapiga hela zaidi kwa endorsements kibao za makampuni ya ndani na nje ya Kenya. 

Ni haki kuwa na walinzi wake binafsi kama hivi. Safi.

Tedd Josiah arejea nchini Kenya, ni baada ya kukimbia mwaka 2008



Producer mkongwe wa nchini Kenya Tedd Josiah amerejea kwenye muziki wa Kenya baada ya kukimbia nchini humo na kutafuta hifadhi ya kisiasa nchini Uingereza kutokana na vitisho alivyovipata kwa kutengeneza tangazo la TV la ‘Domo TV'.

Josiah alikuwa akikipigia debe chama cha ODM na mgombea wake wa urais Raila Odinga.

Wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi nchini Kenya, Josiah alihisi maisha yake yapo hatarini hivyo kwenda jijini London mwaka 2008, na kupotea kabisa kwenye ramani ya muziki nchini Kenya.

Wednesday, August 8, 2012

Shabiki wa Prezzo aimwangia matusi ya nguoni Big Brother Africa



Sylvanus Joseph (shabiki wa Prezzo) ameamua kuipeleka hasira yake dhidi ya ushindi wa Keagan kwenye shindano la BBA Stargmame kwenye level nyingine na kumwaga matusi ya nguoni kwa haters wote wa Prezzo.

“YOU ASS HATERS OF PREZZO GO AND FUCK YOU KEAGAN ACCENT, AND REMEMBER THAT PREZOO IS MORE THAN OF YOUR BOY IN EVERYTHING FROM , MONEY, POPULARITY, TALENT AND EVEN KNOWLEDGE. SA SHOULD THANKS GOD FOR THAT COMPANSATION FROM BIOLA FOR 7YRS LOSS, JUST EVEN WITH A NARROW MIND DO YOU THINK KEAGAN WAS EVEN BETTER THAN LADYMAY/ YOU STUPID PORNSTARS BE KEEN.

PREZZO WILL STILL DO HIS MUSIC AND OWN HIS MINING COMPANIES, MAKINI SCHOOLS, HOUSES AND EVEN THOSE MAKINI HERBALS. OFCOURSE HE IS RICH ENOUGH AND AS HE TOLD YOU THAT HE DOn't CARE FOR 300K USD. HE WANTED TO TELL YOU THAT HE IS THE BOSS AND KENYA IS REAL PLACE TO BE. SHAME ON YOU GUYS WHO ARE THE HATERS.

Sunday, August 5, 2012

Nonini kutangaza kipindi cha asubuhi cha 97.1 One Fm



Nonini atakuwa mtangazaji mwenza kwenye kipindi maarufu cha kituo cha One Fm cha jijini Nairobi kiitwacho One Breakfast kuanzia kesho hadi ijumaa.
Kupitia Facebook, msanii huyo ameandika:

“Social Media has always played a big part in my career...Mimi utreat blog zangu,status updates and tweets kama a communication platform kubonga na ma vijanaa...Its about time we combine all this and take it to the next level. So starting 2morrow from 6am-10am monday mpaka friday i will be hosting the popular Onebreakfast show on 97.1Onefm home of Urban and Local Music Station! I am excited to be part of the 1fm Family and thank my fans WagengeTrue but most importantly God Sir Jah Mwenyewe! RAPPRENUER!”

Friday, August 3, 2012

Pepsi yawamezea mate Camp Mulla



Kampuni ya SBC Kenya Limited imedaiwa kuwamezea mate Camp Mulla ili wame sura za kinywaji cha Pepsi.

Kama ikiwachukua itakuwa na uhakika wa kampeni yake kuwafikia vijana wengi wa Kenya ambao wanalizimia kundi hilo.

Chanzo kimoja kimeliambia gazeti la The Star kuwa Pepsi wanalitaka soko la vijana na  Camp Mulla wako juu sana sasa hivi hivyo hiyo itakuwa ni rahisi kwa kinywaji hicho kuongeza umaarufu kupitia wao.

Camp Mulla linaundwa na vijana watano, Taio Tripper - Matthew Wakhungu, Shappa Man - Benoit Kanema, Miss Karun - Karungari Mungai, K'Cous - Marcus Kibukosya na mwanzilishi Mykie Tuchi - Michael Mutooni.

Sunday, July 29, 2012

Picha: Jason Derulo akiperform nchini Rwanda

Jana mwanamuziki wa Marekani Jason Derulo alitumbuiza kwenye uwanja wa Amahoro nchini Rwanda kwenye fainali za shindano la Primus Guma Guma SuperStar. Hizi ni baadhi ya picha za show hiyo.