Ukitaka kufanya collabo na Lady Jaydee hakikisha kuwa unalibold kulitilia msisitizo neno “uvumilivu” katika kamusi ya maneno yako kichwani.Ratiba yake kwa siku imejaa mambo mengi ya muhimu kuyafanya.
Kikubwa ni mishe mishe ya vitega uchumi vyake vikiongozwa na Nyumbani Lounge na safari za hapa na pale za nje ya nchi.
Kama Godzilla na Dully Sykes imewabidi wasubiri kwa muda kuzipata sauti za dhahabu za nguli huyo wa muziki nchini, kwa underground watazipata kweli?
![]() | |
| Godzilla |
Hata hivyo Godzilla na Dully Sykes wana haki ya kufurahia kwasababu tayari Judith Wambura aka komandoo amejaribu kufix ratiba yake iliyobana kuzifanyia kazi collabo hizo.
![]() |
| Dully |
“Naanza kupunguza foleni ya Collabo kati ya Dully Sykes na Godzilla nianze na ipi??Natatua 1-1 kwa hatua.. Naahidi kuwa dada mwema kwa wote” ametweet.
Foleni anayoisema Jide huenda ina wengine wengi wanaosubiri sauti yake.
Kwa alipofika mwanadada huyu hilo ni jambo la kawaida na anastahili kuvumiliwa.


No comments:
Post a Comment