Wednesday, May 9, 2012

Wapenzi wa zamani wa 50 Cent na Floyd Mayweather wayaweka hadharani madudu ya mastaa hao



Wapenzi wa zamani wa 50 Cent na Floyd Mayweather wameibua mambo mazito yanayohusiana na mahusiano yao na nyota hao wawili ambao ni washikaji.

Shaniqua Tompkin ni mama wa mtoto wa kiume wa 50 mwenye miaka 15 aitwaye Marquise, wakati Josie Harris ni mama wa watoto watatu wa Floyd.

Mshindi huyo wa mkanda wa welterweight aliyeuchukua weekend iliyopita kwa kumcharaza Miguel Cotto anajiandaa kwenda kutumikia kifungo jela mwezi ujao kwa kumshambulia Josie mwaka 2010.
Wanawake hao wamekaa na kuzungumza na mtandao wa Mommysdirtylittlesecret.com, na kuweka hadharani ubabaishaji wa Floyd na 50.

Akiongea kuhusiana na uhusiano na 50, Shaniqua amesema: "Ulikuwa wa kupanda na kushuka . Ni uhusiano mgumu kuuelezea. Ni mkali, mkali sana."
Shaniqua

Anadai kuwa rapper huyo ni baba mbaya na hajamuona mwanae kwa miezi mitano. "50 ni  mhudumiaji mzuri, lakini ni baba mwema? Hapana. 

Hajawahi kuhudhuria hata mchezo mmoja wa mwanae,” anasema. “Tena mara ya mwisho kumuona ilikuwa December. Tulipokuwa pamoja alinisaidia kumkuza binti yangu pamoja na mtoto wetu wa kiume lakini tulipoachana yote yaliisha. 

Hakuwa tena baba wa mtoto wake. Anachodhani yeye kuwa baba ni kutoa matumizi tu, lakini haiko hivyo”

Shaniqua pia anadai kuwa Fiddy alikuwa mgomvi na kuongeza: Ndiyo, alipoamua kunipiga mbele ya binti yangu ndipo nilipotambua kuwa uhusiano ulikuwa umeisha”


Floyd na Josie




















Kwa upande wake Josie, pamoja na hukumu ya kwenda jela aliyoipata baba watoto wake, anasema ameshamsamehe Floyd kwa kumshambulia.

"Floyd Mayweather Jr. is a d***. Nimemsamehe, yamekwisha”

Josie anaamini kuwa mchumba wa sasa wa Floyd Shantel Jackson yupo kwenye uhusiano huo sababu ya pesa.

"Anatawaliwa (Shantel). Acha nikuambie jinsi ilivyo…wametangaza kwenye radio kuwa watafunga ndoa siku ya birthday yangu! C’mon…Anajua (Floyd) anachokifanya na ni mwanamke gani anayekubaliana na hilo?
Floyd na Shantel




No comments:

Post a Comment