![]() |
Chameleone |
Chochote atakachokitaka Jose Chameleone atakipata.
Wiki iliyopita nyota huyo wa Valu Valu alichukia vibaya baada ya gazeti la New Vision la Uganda kuandika kuwa msanii wa kike wa Hip Hop nchini humo Keko alikuwa anapendekezwa zaidi kati ya wasanii watatu wa Uganda watakaoshare stage moja na mwanamuziki wa Marekani na member wa kundi la Dru Hill Sisqo,ambaye atafanya show mjini Kampala mwezi wa nane mwaka huu.
![]() |
Keko |
Baada ya hasira hizo alichofanya Chameleone ni kuwapigia simu mapromota wa kimataifa wenye makazi yao nchini Uingereza Chinedu Ikoroha na Misairi Kabira na kubadilisha kila kitu.
Hawakuwa na la kufanya zaidi ya kusikiliza pia ushauri kutoka kwa washauri wa hapo hapo Uganda.
Mpaka sasa Jose Chameleone ndiye msanii wa Uganda pekee aliyethibitisishwa kutumbuiza mbele ya Sisqo wakati nafasi ya Keko ikibaki matatani.
![]() |
Sisqo |
Come on Chameleone! Juzi tu umezindua simu zako za mkononi ikiashiria kuwa hela unayo, kwanini umbanie binti wa watu kupata mchongo huo naye akapiga mavumba!
No comments:
Post a Comment