Wednesday, May 9, 2012

Navio ashinda tuzo barani Asia




























Nyota ya rapper Navio kutoka Uganda inang’aa mbali ya bara la Africa. 

Habari mpya kuhusiana na msanii huyo wa Hip hop ni kuwa ameshinda tuzo kubwa zilizotolewa nchini Malaysia.

Navio, ambaye hivi karibuni alikuwa Kuala Lumpur, ameshinda kipengele cha Best East African Act katika tuzo za African Entertainment.

Hizi ni tuzo za thamani barani Asia kusherehekea malengo yaliyofikiwa na waafrika katika tasnia ya burudani katika vipengele vya muziki, sanaa, filamu, michezo, vyombo vya habari, matukio na mambo mengine ya kijamii.

Katika tuzo hizo, hayati Lucky Dube alishinda tuzo ya Lifetime Achievement.

Miongoni mwa wasanii walioutumbuiza ni pamoja na  yeye mwenyewe Navio, Awilo Longomba na Nkulee Dube, binti wa  Lucky Dube.

Wabongo mpooo? 

No comments:

Post a Comment