Monday, May 14, 2012

Show za makampuni furaha kwa wasanii, kilio kwa mapromoter!




Jumamosi hii ile kampeni ya #OneBillionReasons2Believeinaangukia jijini Arusha. Maswahiba AY na MwanaFA ndo watakaotumbuiza.

Kiingilio walaa hakishtui, ni Coca yako tu mkononi  halafu unachoma ndani kula raha!

Hapo AY na MwanaFA wana mshiko wao saaafi kutoka kwa Coca usiokuwa na mawazo. Hela ipooo hakuna kubargain ili kushushana bei. 

Kinachofanyika ni call moja tu kwa msanii “Ebwana AY eeh! tunashow Arusha jumamosi njoo uchukue ‘milioni tano yako’ kesho usaini kabisa na mkataba!

Aaaaah! Habari imekwisha hiyo. Sasa tujiulize swali! Yule promoter jamaa yetu ambaye yeye hutegemea deal hizo ili watoto waende shule atampata AY kweli? 

Hata kama anaweza kumlipa hela atakayotaka, atairudishaje hela yake kwa kiingilio cha shilingi 5,000 wakati juzi tu AY alikuwa huko huko na kiingilio kilikuwa Coca moja tu? Utamshawishi vipi shabiki kulipa elfu tano wakati msanii huyo huyo alimwona kwa shilingi 600 ya soda? Kwanini promoter asianzishe tu biashara nyingine ama kurudi kijijini kulima mpunga!

Makampuni kama haya hayana shida na hela za mashabiki. Hela ipo tayari. Yanachotaka ni kuitangaza tu bidhaa yao kwa njia ya burudani na kwa kuwalipa fedha lukuki wasanii ili mashabiki ambao ni wateja wao pia waendelee kuutambua uwepo wa bidhaa zao na kuendelea kuzinunua.

Makampuni makubwa hayaoni tabu kuchukua wasanii kumi na kuwalipa milioni 2 ama 3 kila mmoja na watu wakaingia bure!

Wakati hili likiendelea mapromoter wenye mitaji midogo wamejikuta wakishindwa kumudu kuandaa tena show kubwa. 

Watu pekee waliobaki na ubavu wa kufanya hivi ni wafanyabiashara wakubwa ama radio zinazoandaa matamasha kwa support ya wadhamini.Show za kiingilio sasa hivi zimekuwa ngumu mno ndo maana watu wanakula za uso sana siku hizi. Ili kufanya show ilipe lazima iwe na mashamsham mengi!

Wakati huo ambao mikakati ya masoko(marketing) kwa makampuni makubwa imejiingiza sana katika kuhusisha wasanii na kufanya show za bure, wasanii wamejikuta wakinufaika sana lakini kuwaacha mapromoter hoi wakipumulia mashine.

No comments:

Post a Comment