Rappers wa kike nchini Marekani akiwemo Nicki Minaj wakae chonjo kwasababu Serena Williams amekuja kuwaonesha kuwa sio tenesi tu inayoweza kumpa ugali mezani bali pia yuko poa kwenye michano.
Kwa mara ya kwanza amekuja na wimbo wake mpya na kwa taarifa yako, hasikiki kama anajifunza, mwanadada yuko fit.
Mtandao wa TMZ ndio ulioisanua story yenyewe. Serena kafanya ngoma kadhaa kwenye studio iliyopo Florida iitwayo B Major Music Group inayomilikiwa na mchezaji wa timu ya football ya Baltimore Bryant McKinnie ambaye ni rafiki wa karibu wa kinadada wa Williams.
Na sasa tayari miongoni mwa ngoma zake zimeshasambaa shambani (internet) na walioivuna wameshangazwa na uwezo wa mchezaji huyu maarufu wa tenesi.
Infact, sisi wenyewe tumemkubali.
Kwa uwezo wake huu kama akiamua kujitosa mzima mzima kwenye game, akina Nicki Minaj na wengine wamepata mshindani wa kweli.
Hebu msikilize:

No comments:
Post a Comment