Friday, May 11, 2012

John Cena kumpa talaka mkewe licha ya kumpiga busu hadharani March mwaka huu



























Miezi miwili iliyopita katika WWE Raw John Cena alimwangushia busu zito mke wake aliyekuwa amesimama sehemu ya watazamaji kumshangilia mumewe anavyofanya mambo ulingoni.
Kwa wengi kitendo hicho kilionesha wazi kuwa ndoa yao iko thabiti na mahaba yamepamba moto!

Waswahili husema usilolijua ni sawa na usiku wa giza! Mpaka unaisoma habari hii ni kwamba tayari mcheza mieleka huyo kipenzi cha wengi amewasilisha ombi la kumpa talaka mke wake Liz Huberdeau aliyedumu naye kwa karibu miaka mitatu.



























Swali kwa wengi ni kuwa uamuzi huu utaathiri performance yake ulingoni?

Watu wa karibu naye wamedai kuwa miezi ya hivi karibuni John amekuwa akionesha hana mzuka kabisa licha ya kumwangushia busu zito mkewe tarehe 5 mwezi March live bila chenga kwenye TV.

No comments:

Post a Comment