Friday, May 11, 2012

Nicki Minaj na boyfriend wake kuzaa? Miaka mitano ijayo!


Nicki Minaj amethibitisha kuwa anataka kutulia na kuanza kulipa uzito suala la kuwa na watoto miaka mitano ijayo.

Kwa sasa rapper huyo ‘mapepe’ ana uhusiano na meneja na rafiki yake Safaree aka Scaff Beezy, na tayari wapenzi hao wamedaiwa kuchumbiana.

Wait a minute! Si juzi tu hapa Big Sean amesema ameula mzigo wa Nicki! Kama ni kweli basi Safaree ni wale wanaume 'mabwege' na hana sauti kwa Nicki. Na mara kibao wapenzi hawa wa aina yake wamekuwa wakigombana na asubuhi ya kesho yake utawaona pamoja tena.


"Labda ntakuwa na mtoto. Ningependa kuzalia hapa hapa kwenye show yako” Nicki amemwambia  Ellen Degeneres kwenye show yake baada ya kuulizwa atakuwa anafanya nini katika miaka mitano ijayo.

No comments:

Post a Comment