Saturday, May 12, 2012

Ridhiwan awapiga 'dongo' wasomi waliopigika!



Hivi hujawahi kushangaa mtu unayemjua kuwa ni msomi wa hali ya juu, kwa mfano anaweza kuwa na masters ama Phd lakini  amepigika kinomanoma! Mtu huyu anaweza kuwa na kazi nzuri sehemu, yenye mshiko wa maana lakini hana lolote! Hata baiskeli! 

Ama hujawahi kuhudhuria mazishi ya mtu aliyekuwa msomi na mwenye wadhifa mkubwa serikali lakini nyumbani kwao anapozikiwa wazazi wanalala na mbuzi kwenye nyumba moja? 

Ofcourse wapo wasomi ambao wamesoma fani zisizolipa kwa mfano Daktari wa mifugo! Kibongobongo fani hii hailipi kivile na ndo maana Hermy B msomi wa fani hiyo kutoka SUA, aliamua kuipotezea baada ya kuona kaingia 'chaka' na kuelekeza nguvu zake kwenye production ya muziki kitu ambacho kinampa mkate wa kila siku. Mkate mnono haswaaaa!

Tuachane na blah blah hizo na tuuangalie mchongo kamili. Ridhwan Kikwete ameamua kuwaasha wasomi wa aina hiyo!


What a waste! Yeah jamaa kasema ukweli. Hata hivyo kuna sababu nyingi zinazomfanya msomi awe broke. Sababu ya kwanza ni kama tulivyoeleza hapo juu. Lakini kwa nchi kama Tanzania kukutana na wasomi waliopigika ni kitu cha kawaida kama makofi polisi.

Wasomi hawalipwi wanavyostahili na ndo maana wengine kama madaktari huamua kugoma kudai ujira zaidi. Na wengine huona isiwe tabu na kuamua kwenda kutafuta maisha nchi za wenzetu ambao huwajali zaidi wasomi.

Hivyo Bwana Ridhiwan kabla hajasema “A broke intellectual. What a waste! amwambie kwanza 'mshua' awaongezee ujira wasomi hawa waliopigika.

No comments:

Post a Comment