Kwa watembeleaji wa mitandao ya kijamii kama Facebook na Twitter bila shaka wameshakutana na tangazo hili hapo chini:
Ni show ya mkali wa Dancehall na kipenzi cha masista duu, Sean Paul kutoka Kingston,Jamaica itakayofanyika May 17, Wichita,Kansas nchini Marekani.
Tamasha hili lina faraja pia kwa wapenzi wa muziki wa Tanzania. Ni katika show hiyo kijana mwenye kipaji kutoka Bongo ambaye si mgeni kwa wengi atashare stage moja na mkali huyo.
Si mwingine ni Stanboi aka the African Child.
Kupanda stage moja na Sean Paul si kitu rahisi kama CV yako inachechemea. Lakini pia mjini Wichita kuna wakali wengine hivyo swali ni kwamba Stanboi amepataje shavu hili?
Tumemtafuta na kuzungumza machache kuhusiana na show yenyewe na namna anavyojisikia.
Leotainment:Kwanza kabisa, tuambie umepataje nafasi hii?
Stanboi:Kuna kituo cha radio huku Kansas kinachoitwa Power 93.9. Radio hii huandaa show zote kubwa na pia hucheza nyimbo zangu. Kila wanapokuwa na show kubwa hunipa nafasi ya kutumbuiza na wasanii wakubwa.
Leotainment:Unajisikiaje kupata fursa ya kuwa kwenye stage moja na Sean Paul?
Stanboi: Najisikia poa mno kuwa kwenye stage moja na Sean Paul kwasababu nafasi kama hizi huwa haziji kirahisi.
Leotainment:Umeshawahi kushare stage moja na wasanii wakubwa kama Mims, Chameleonare, Baby Bash, Kreayshawn na wengine wengi, Je! Huwa hauingiwi na woga?
Stanboi: Huwa naingiwa na wasiwasi kwa sekunde 5 tu kabla sijapanda stejini. Nikishakuwa kwenye stage, kila kitu hubadilika na kuanza kujisikia kama namiliki sehemu yote pale na kufanya show ya ukweli sana. Kuwa na wasiwasi ni sehemu ya kujiweka tayari kwa ajili ya kufanya show nzuri.
Leotainment:Unajisikiaje kuwa miongoni mwa wasanii wachache kutoka Tanzania kushirikishwa kwenye show kubwa za aina hiyo?
Stanboi: Najisikia safi sana kuwa miongoni mwa wasanii kutoka Tanzania wanaoshiriki kwenye show hizi inaonesha kuwa popote kule unapotoka ama unachofanya, kama tu ni unafanya kazi nzuri, siku zote watu watakuheshimu na wewe utapata fursa kubwa. Wakati huo huo, inapendeza kwasababu wananitambua mimi kama msanii kutoka Afrika Mashariki. Naiwakilisha nchini yangu, na ni hisia safi sana.
Leotainment:Kitu gani watu wategemee kutoka kwako?
Stanboi: Ningependa mashabiki wangu watambue kuwa naachia EP yangu ambayo itakuwa na nyimbo sita katika kipindi cha kiangazi mwaka huu na pia nitazindua nembo/biashara yangu mwenyewe inayoitwa The African Child. Mambo mazuri yako mbioni kutokea kiangazi hiki na ninaamini mashabiki wangu wako tayari kwa hilo. Tanzania, stand up!
Mashabiki wake wanaisubiria kwa hamu show hiyo kama huyu anavyosema:
Mwangalie hapa alivyoperform miezi sita kwenye show aliyopanda stage moja na Mims,Baby Bash, Kreayshawn na Mann.
No comments:
Post a Comment