Wiki hii Izzo B ameachia ngoma mpya iitwayo Mwaka jana (Nakuchukia). Humo kaongea mengi ya kwanini anauchukia mwaka 2011.
“2011 nakuchukia, ulifanya niporwe demu kisa pesa sikuwa nayo.
Zilizagaa kila sehemu konde nilipiga moyo
Ulimtesa baba yangu kutokushinda mahakani
Ulivuruga ubongo wangu chuo sikutamani
Mwakyembe akawa hoi na sichoki kumuombea
2011 naapa nakuchukia Mr Ebbo kama ndoto leo hatuko naye” ni miongoni mwa mashairi katika wimbo huo.
Kwa wapenzi wa filamu nchini wana haki ya kusema mwaka 2012 ni mwaka mbaya kabisa kuwahi kutokea.
Mwaka huu umekuwa mchungu kwa waigizaji wengi wa filamu. Kwanini?
1. Kifo cha Stephen Kanumba
Mwaka huu Tanzania imeshuhudia pigo la kuondokewa na muigizaji maarufu na anayependwa aliyewahi kutokea katika historia ya filamu nchini Stephen Kanumba. Kwa namna alivyokuwa ameiweka Tanzania katika ramani ya filamu barani Afrika, pengo lake litachukua muda kuzibika ama halitazibwa kabisa.
2. Kukamatwa kwa Elizabeth “Lulu” Michael
Kifo cha Kanumba mwaka huu hakijaacha pengo kubwa kwa mashabiki wake pekee, bali pia kimeziharibu ndoto za msichana Lulu aliyekuwa mpenzi wake na ambaye kwa sasa yupo mahabusu kwa tuhuma za kusababisha kifo cha Kanumba.
3. Kuugua kwa Sajuki
Kuugua kwa Juma Kilowoko aka Sajuki ni pigo jingine tena.
Ugonjwa wake umembadilisha Sajuki yule kipenzi cha wengi kwenye filamu. Na sasa baada ya jitihada za mke wake Wastara na wadau wengine, wamefanikisha kupata fedha za matibabu yake nchini India.
4. Kajala kuwekwa rumande
Kajala Masanja naye mwaka huu amejikuta mahabusu kwa kukabiliwa na mashtaka ya ufujaji wa pesa za umma zinazomkabili yeye pamoja na mume wake.
Yeye na mume wake Faraja Chambo, wanakabiliwa na makosa matatu, kosa la kwanza ni la kula njama kinyume na kifungu cha 34 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya mwaka 2007, ambapo washtakiwa wote kwa pamoja walitenda kosa hilo la kula njama la kuhamisha umiliki wa nyumba iliyoko Kunduchi Salasala, eneo ambalo halijapimwa jijini Dar es Salaam.
Tuombee Mungu arudishe tena utulivu na amani katika tasnia ya filamu nchini inayofanya vizuri kwa sasa.
No comments:
Post a Comment