Wednesday, May 9, 2012

VERY EXCLUSIVE: Mtanzania aishiye Czech aelezea video shoot ya wimbo wa Kanye West na Jay-Z!




















Jana (May 8) tuliweka vipande kadhaa vya video vilivyoenea kwenye mtandao wa YouTube vinavyodaiwa kuwa vimetoka kwenye video shoot ya wimbo wa Kanye West na Jay-Z  'No Church in the Wild.'

Video hizo ambazo zimechukuliwa mjini Prague, Czech Republic wiki moja tu iliyopita vinawaonesha waandamanaji waliovaa mask na polisi wakipambana katika mitaa ya mji huo iliyoharibiwa.

Mmoja wa wadau wetu wakubwa aishie Jamhuri ya Czech ambaye ni daktari kutoka Tanzania aishie huko Mahundi, E.P.F ametumegemea data exclusive kuhusiana na video hiyo.

Mahundi
“Huyu jamaa Kanye(and many other U.S movie stars and musicians) wamekuwa wakishootia sana video na movie zao hapa Czech, coz its ten times cheaper for them and the country is very beautiful....especially wanapotaka kushoot video kali au ndefu. 

Hata video yake ya Runaway aliifanyia hapa Prague, na wale watu walio pale weusi wote ni wanafunzi kutoka nchi mbalimbali za Africa kama Congo, Kenya S.A, Guinea...and i know them personally...so you know why the costs are cheaper for them here” anasema.


Leotainment ilitaka kujua ni kiasi gani wahusika wote waliochukuliwa kuonekana kwenye video hiyo walilipwa ambapo Mahundi anasema: “Hawa jamaa ambao wanaact kama xtras au compass kwenye background huwa wanalipwa approximately 1500-2000 Czech crowns (CZK) per shooting day..

1CZK ni kama Tshs 80, so ni kama 120,000 -160,000 Tshs kwa kila shooting day. Inategemea wanashoot how many days.Ila characters wengine muhimu kama atakayeact kuwa demu wake as in runaway analipwa pesa nyingi, na ni personal negotiations".

Tulitaka pia kujua actors huwa wanapatikanaje na Mahundi anaendelea kufafanua: “Wanapatikana hivi, hapa kuna casting agencies e.g. extra films...so watu wanakuwa wamejiregister kwenye hiyo agency. Yeye Kanye akija anatafuta agency anawaambia anataka watu kadhaa na wa aina hii...e.g 20 blacks and the rest can be any.

So agency inaanza kuwacall na kuchagua watu waliojiregister hapo kuwa ebwana kuna mzigo hapa, njoo upige. Wakienda bado Kanye pia atawachagua na kuwachuja wale ambao anaona wanafaa kuwa kwenye video yake. Lakini yeye anailipa agency kwa tuseme 4000 CZK per mtu, ila agency nao wanakula cha juu....kwa marekani cost ya kushoot the same video wud be almost tenfolds...”


Kwa waliziona clips hizo bila shaka wanajiuliza kama mitaa ya mji wa Prague ilifungwa kupisha kazi hiyo ama vipi, Mahundi anafafanunua: “Hiyo mitaa kama kuna shooting basi ni kweli inafungwa. Ni shooting tu inaendelea, maana wanakuwa wamepewa shooting permit/licence na Prague city.

Hapa Jamhuri ya Czech zimeshootiwa movie nyingi sana, mfano Casino Royale, Blade 2 , kuna movie ya Chris Rock, Last Holiday ya  Queen Latifah, etc.

Hiyo Jungmanovo street iko karibu na Wenceslaus square ambayo ndo the heart of prague.

Jungmanovo street



















Wenceslaus Square 





















"Prague imegawanywa into prague 1-10, so hapo ndo prague 1” Anasema Mahundi.

No comments:

Post a Comment