Showing posts with label NEW MUSIC. Show all posts
Showing posts with label NEW MUSIC. Show all posts

Friday, August 10, 2012

New Music Video: G Nako ft. AY & The Artist - Take Off





Hongera kwa G Nako kwa kutake ‘risk’ kufanya ngoma na video hii. Ili kuweza kuelewa lengo lake la kuamua kufanya wimbo wa aina hii inabidi ufikirie ‘globally’ zaidi.Kwa maana kwamba hizi ni video ambazo ni rahisi kupata airplay kwenye vituo vikubwa vya runinga duniani hususan Channel O, Trace TV  na MTV Base ambazo zimetawaliwa na wanamuziki wa Nigeria na Afrika Kusini zaidi. 

Kwa wapenzi wa muziki wa Tanzania waliozoea kulishwa muziki wa aina moja wanaweza kusema G Nako amechemka lakini lahasha, hajachemka hata kidogo! He is on point. Hii video inaweza kuanzisha status mpya ya G Nako kama mwanamuziki wa kimataifa kwa maana ya kuanza kujulikana katika nyingi za Afrika kama ilivyo kwa AY na wasanii wengine wachache wa Tanzania.

Kuna taarifa kuwa label ya Sony Music Group Africa inataka kuwasaini wasanii kibao kutoka Afrika Mashariki na jana label iliyopo chini yake, ROCKSTAR4000 kupitia Twitter na Facebook iiliandika, “Another HOT HOT signing from East Africa to Sony Music Entertainment and ROCKSTAR4000... Who do you think it is??? (watch this space...)”. 

Kwa maana hiyo wasanii watakaopata mchongo huu kutoka Tanzania lazima waoneshe uwezo wa kuuzika kimataifa kama ilivyo kwa AY sasa hivi.

So big up kwa G Nako kulitambua hilo mapema.

Thursday, August 2, 2012

New Music - May C - RudeGalz


May C mwanadada kutoka Arusha amekuja kivingine na ngoma yenye mchanganyiko wa dancehall na rap, Rudegalz.

Hii ni ngoma ya kuparty zaidi na inayoonesha uhuru kwa mwanamke ambaye anatafuta cash mwenyewe ambazo zinamfanya atoke bila kutegemea support ya mwanaume.

Anasound sexy sana anaporap na ukilinganisha na urembo wake, ngoma za aina hii zinaweza kumpa nafasi zaidi Bongo sababu ni wasichana wachache nchini wanaofanya ngoma za aina hii.

Ngoma imefanya na DefXtro wa NoizMekah. Nice tune for real!
 

New Music: Navio ft Nonini, Chameleon & Uganda All Stars – Dream Remix


New Music: 2face, D'banj, M.I Abaga, Wizkid & Tiwa Savage - Let's Get This Party Started


Tuesday, July 10, 2012

New Music: Suma Mnazaleti ft.Ommy Dimpoz - Chukua Time


New Music: Sheila Kwamboka (BBA 2008 na 2010) - Yours




Kwa wapenzi wa Big Brother jina la Sheila Kwamboka aka Kwambox sio geni. Alianza kujulikana mwaka  2006 aliposhinda taji la Miss Tourism Kenya. Baada ya hapo alifanya kazi kama ripota kwenye kituo cha runinga nchini humo mwaka 2008.

Mwaka huo huo akaiwakilisha Kenya kwenye Big Brother Africa na kisha kurejea tena mwaka 2010 kwenye Big Brother Allstars.

Kwa sasa anafanya muziki, muigizaji na muongozaji wa filamu.