Vipande kadhaa vya video vimeenea kwenye mtandao wa YouTube vinavyodaiwa kuwa vimetoka kwenye video shoot ya wimbo wa Kanye West na Jay-Z 'No Church in the Wild.'
Video hizo ambazo zimechukuliwa mjini Prague, Czech Republic wiki moja tu iliyopita vinawaonesha waandamanaji waliovaa mask na polisi wakipambana katika mitaa ya mji huo iliyoharibiwa.
Ripoti kwenye website moja ya nchini Slovakia imedai kuwa uchukuaji wa video hiyo umefanyika kwa siku 3 katika mtaa wa Jungmanova na Legion Bridge ambapo gari ya polisi ililipuka kama sehemu ya ‘stunt’ kubwa ya scene hiyo.

No comments:
Post a Comment