Unamkumbuka Teddy Kalonga aka TK? Model wa kimataifa aishie Hollywood, California nchini Marekani.
Kwa sasa ni mama wa mtoto mmoja. Kuwa mama hakujazirudisha hustle zake katika showbiz!
Katika page yake ya Facebook kuna picha zikimwonesha akiwa studio tayari kuingiza sauti!
Maswali yamekuwa mengi kutoka kwa rafiki zake akiwemo Lady Jaydee ambaye ameuliza, “Unaimba bi dada?”
Pamoja na kuwa hajajibu lolote tumeweza kufuatilia picha zake za nyuma na kukutana na picha ya mwaka 2010 kwenye blog yake mwenyewe akiwa studio na kuandika “K: "Just recently after being back from my home country Tanzania, straight up got back to business. Shown on the pictures, me doing a television voice over for an ad in Los Angeles earlier this week". Praise the Lord Jesus Christ!i
Maelezo hayo yametupa jibu kuwa kuonekana kwake studio kunamaanisha kuwa anaingiza sauti ya tangazo,documentary ama mambo mengine yanayohusiana na TV.
Pia inatupa jibu kuwa hajaiacha kabisa fani yake ya utangazaji iliyompa jina nchini kwakuwa mmoja kati ya waanzilishi wa Channel 5!
![]() |
TK na familia |
No comments:
Post a Comment