Monday, May 14, 2012

Mfahamu Peter Ligate anayewapeleka wasanii wa Bongo Marekani


Peter Ligate



















Kila siku umekuwa ukisikia msanii wa Bongo ameenda Marekani kupiga show na anakaa huko kwa miezi. 

Ulishawahi kujiuliza ni nani huwa anawapeleka? Sasa hivi ameendela Linah na kila siku kwenye blogs mbalimbali unaona picha zake mtoto akila bata tu kwa Obama.

Nani huyu anayeziwezesha show hizi?

Ni Peter Ligate. Mtanzania aishiye Marekani. Ni msomi katika chuo kikuu cha Westminster, London katika fani ya  Electrical Engineering  na University of Maryland, College Park akichukua MSc Telecommunications.

Kwa sasa ni Rais na Mwenyekiti mtendaji wa  J & P Investments Inc. Peter anasema alikuja Tanzania katika safari zake za kawaida kusalimia ndugu na jamaa mwaka 2003 ambapo alikua hajui chochote kuhusu Bongo Fleva. Lakini alishangaa kila kona alikokuwa akipita alisikia nyimbo za Bongo Fleva na zikamvutia.

"Nikasema hiki kitu ambacho mimi napenda na nafikiri ni kitu kizuzri ambacho sasa hivi nyumbani wamekipenda na wamekipokea vizuri kwanini na ndugu zangu wa huku Ulaya wasipate nao hiyo nafasi” anasema.

Na hapo ndipo Ligate akaanza kuwapeleka wasanii akiwemo Mr.Nice na kufanya show Marekani huku nia yake pia ikiwa ni kuutaganza muziki wa Tanzania.

Leotainment imemtafuta Ligate na kuzungumza machache kuhusiana na concerts anazoziandaa pamoja na mipango ya baadaye.

Leotaiment: Umefanikiwa kuwapeleka wasanii wakubwa wa Bongo na kuperform Marekani na kwingineko, hauna mpango wa kuleta wasanii wa Marekani Tanzania ili kuwapa fursa wapenzi wa muziki wa nyumbani kuwaona wasanii wawapendao?

Ligate: Kwa sasa sina mpango huo..kwani tayari wapo wanaoleta wasanii wa Marekani huko na isitoshe tayari wamarekani wameshafanikiwa kwa kiasi kikubwa. Mimi lengo langu kuu kwenye hili swala zima ni kuchangia sanaa yetu ya Bongo Fleva, kama nilivyoeleza hapo awali kulikuwa hakuna mtu ambaye alikuwa analeta wasanii hao hapa Marekani na niliona kuwa watanzania wengi wa huku ulaya ni vizuri wapate hiyo fursa ya kuburudika na mambo ya nyumbani.

Leotainment:  Mara nyingi wasanii unaowachukua kwenye show zako hukaa huko kwa muda mrefu kidogo na hiyo ni gharama kubwa,hufikirii siku moja kuja kufanya show moja kubwa huko Marekani na ukachukua wasanii wengi wa Bongo, tuseme zaidi ya kumi kwa wakati mmoja?

Ligate: Hiyo ni ndoto yangu kubwa sana.  Nina mpango wa kuandaa tamasha kubwa la aina yake siku za usoni. Ninajipanga kutafuta wahisani wa kunisaidia kwani swala kubwa kama ulivyo sema ni gharama kubwa.

Leotainment: Ni msanii gani katika wote ulioawahi kuwachukua aliyezikonga zaidi mioyo ya mashabiki wa huko?

Ligate:Kusema kweli ni wote wamefanya vizuri sana. Kama unavyoona nimekuwa nikifanya kazi na watu tofauti mfano Mr.Nice, Ali Kiba, Professor Jay walikuwa wanaume na zaidi wameegemea kizazi kipya, vile vile nilibahatika kufanya kazi na Khadija Kopa ambaye alitupa mambo ya pwani, mzee wetu King Kiki alitupa burudani ya kiutu uzima na sasa nikaona ni wakati mwafaka nifanye na msichana wa kizazi kipya ambaye kwa sasa ni Linah ambaye anatisha huku Marekani.
Leotainment:Audience inayokuja kwenye matamasha unayoandaa inajumuisha watanzania tu ama kuna watu wengine kutoka Afrika ambao huhudhuria?

Ligate: Kwa sasa imekuwa zaidi watanzania na watu wa Afrika Mashariki ndiyo ni wengi ingawa tunapata watu wa nchi zingine ambao huwa na wao wameanza kujitokeza.

Leotainment: Licha ya matangazo katika websites na blogs, ni njia nyingine zipi za promotion huwa unazitumia kutangaza show hizo?
Ligate:Tunatumia sana sms (text), radio zinazo rusha mambo ya kiafrika, mapostas, flyers, kuambiana mtu mmoja mmoja n.k.

Linah akitumbuiza Marekani
Leotainment: Katika miaka mitano ijayo unahisi J&P Investments itakuwa inafanya nini?

Ligate:J&P Investments ni kampuni inayojihusisha na mambo ya uwekezaji katika sekta tofauti, kwa sasa tumeegemea sana kwenye real estate (mambo ya nyumba) pamoja na mambo ya burudani. Hivyo basi mwenyezi Mungu akisaidia tutaendelea kuboresha haya mambo makuu mawili, maana watu wategemea matamasha ya nguvu. Vilevile tunategemea kujiingiza kwenye filamu zetu, kuleta documentaries za mambo mbali mbali kuhusu maisha ya huku ughaibuni, kuanzisha talk shows n.k.

Kwa upande wa mambo ya nyumba tunategemea kuja kuleta utaalamu wetu kwenye hii sekta na vile vile kuwekeza kwenye nyumba za kukaa hasa hasa watu wa kipato cha kati pamoja na kuwasaidia watu wa huko nyumbani wanaotaka kununua nyumba au majengo huku Marekani.

No comments:

Post a Comment