Monday, May 7, 2012

Stella Mwangi azimia mara kumi kwa mazoezi ya Beachboy Insanity


STL



















Dunia inabadilika kwa kasi na watu wanagundua vitu kila kunapokucha. 

Unavifahamu vile vipindi vya kwenye TV vya mazoezi ya asubuhi? Anakuwepo mtu kwenye gym akiwapa maelekezo ya mazoezi watu mbalimbali waliojiandikisha.

Sasa hivi zipo DVD maalum zenye maelekezo hayo ya kufanya mazoezi. Kampuni ya Marekani Beachbody LLC inajulikana kwa kazi hiyo ya kutengezea DVD za aina hiyo na bidhaa yake maarufu sana ni Tony Horton's P90X ambayo matangazo yake yameenea katika vituo vingi vya TV.

Rapper wa kike kutoka Kenya Stella Mwangi aka STL anayeishi Norway hajaachwa nyuma na DVD hizi.

Hata hivyo kutokana na ugumu wa mazoezi yenyewe kuwa magumu, imemcost!
 

Alikuwa akijaribu kufanya mazoezi ya DVD iitwayo Insanity na kujikuta akizimia zaidi ya mara kumi.

“Daaaamn! Tried workin out to #BeachBody insanity.. I fainted like 10 times” alisema STL.

Unachotakiwa kufanya ni kufanya mazoezi kwa dakika 3 ama 4 tu kisha unapumzika lasivyo lazima utazimia kama STL.

Insanity inasemekana ni program ngumu zaidi ya mazoezi kuwahi kuwekwa kwenye DVD.

Hakuna vifaa vya kunyanyua ama vingine vinavyohitajika ila mazoezi yake ni magumu na mwili utachoka kiasi ambacho hujawahi kujisikia.

No comments:

Post a Comment