Ikiwa tayari majina ya wawakilishi wa Big Brother Africa Stargame kutoka Tanzania Hilda na Julio yameshajulikana, macho na masikio ya watanzania wengi sasa hivi ni katika hatma yao baada ya kutajwa wa kwanza kuwa hatarini kutolewa.
Awali Jokate Mwegelo alikuwa akitajwa huenda akawa mmoja wa wawakilishi lakini sasa ukweli upo wazi. Kuna jambo moja lakini Jokate anapaswa kujisifia kwa kulifanikisha katika uzinduzi wa mashindano hayo uliofanyika Jumapili.
![]() |
| Flavia na IK |
Vazi alilolivaa mmoja wa watangazaji (host) wa uzinduzi huo Flavia Tumusiime wa Uganda, alilibuni.
Sifa nyingi zimemwendea Jokate kwa kazi hiyo na huenda zikamfungulia njia katika career ya ubunifu wa mavazi.
“Ndio, mtangazaji mwenza wa BBA7 alivaa vazi la Kidoti. Nawashukuru waandaji wa show hiyo kwa kunikubalia” Jokate alitweet.
Jokate ni mtangazaji mwakilishi wa Tanzania katika kituo cha runinga cha Channel 0.
Ulilionaje vazi hilo?


No comments:
Post a Comment