Monday, May 14, 2012

Hatimaye Ali Kiba ajiunga na twitter






















Bado hujajiunga na twitter? Ama umejiunga juzi na bado hujazoea? Basi hauko peke yako. Watu wengi tu bado hawaujui vizuri mtandao huo wa kijamii wakiwemo hata wale usiowategemea.

Heri yake Ali Kiba aliyeamua kujikomboa na kuungana na wasanii wengine wengi wa Bongo Fleva waliojazana kule. 

Kwa mara ya kwanza Ali Kiba leo ameonekana akitweet kwa kuandika wale anaowafuata mpaka sasa. Mpaka jioni saa kumi za jioni jumatatu hii, single boy huyo alikuwa ameshatweet mara nane, followers 66 na anaowafollow wakiwa 55.

Wakongwe katika mtandao huo addictive wamemkaribisha Ali Kiba huku wengine wakimalizia na kichekoo!

Katika wakati huu tuliopo sasa, licha ya msanii kujitahidi kuwa na akaunti facebook, ni muhimu zaidi kwao kujiunga na twitter kwasababu huko ndiko wasanii wengi hutumia muda mrefu kupiga soga.

No comments:

Post a Comment