Baada ya kusambaratika kwa label ya D’Banj na Don Jazzy, Mohits Records ya nchini Nigeria, Don Jazzy amefungua label yake mpya.
Ameitangaza label hiyo itakayojulikana kwa jina la Mavin Records kupitia twitter.
Tayari Don Jazzy amemsainisha mkataba katika label hiyo msanii wa kike wa kimataifa kutoka nchini humo Tiwa Savage.
Ukimtoa mdogo wake D'banj Kayswitch, wasanii wengine wote waliokuwa chini ya Mohits records sasa wamehamia Mavin Records.
Wasanii hao ni Wande Coal, Dr Sid na D’Prince ambao Jumanne hii May 8 wakiwa na Tiwa Savage wataachia compilation album iitwayo Solar Plexus iliyotayarishwa na Don Jazzy.


No comments:
Post a Comment