
Bila shaka umeshaisikia habari ya kuibuka kwa mtu anayejifanya Hayati Daudi Balali aliyekuwa Gavana mkuu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) katika mtandao wa twitter.
Mtu huyo ambaye bado ameendelea kuzisumbua akili za watu, haoneshi dalili zozote za kuacha mchezo huo ambao kwake anaonesha kuufurahia sana.
Tunaamini kuwa Balali alifariki dunia tarehe 16.05.2008 huko Boston, Marekani na kuzikwa huko huko.
Mtu huyo ambaye tayari ana wafuasi 1,651 katika mtandao huo jumatatu hii ameandika “waliokufa hawaongei, wakiongea, basi hawajafa”
Watumiaji wengi wanaomfuata wameendelea kufurahia kumkejeli mtu huyo kiasi cha kumdokezea pia kuhusiana na kuteuliwa tena kwa Abdallah Kigoda kwenye baraza la mawaziri.
Suala la kuibuka kwa watu wa aina hiyo katika mitandao ya kijamii si geni na wengine hutumia majina ya watu maarufu kwa ajili ya kufanya utapeli.



No comments:
Post a Comment