Thursday, May 10, 2012

D'Banj ampongeza Don Jazzy kwa kuanzisha label mpya




Masaa machache tu baada ya producer Don Jazzy kuanzisha record label mpya baada ya kuvunjika kwa Mo'Hits, D'Banj amempongeza wazi bosi wake huyo wa zamani.


Nguli hao waliokuwa wakimiliki Mo'Hits Records walivunja uhusiano wao wa miaka tisa mapema mwaka huu ambapo jitihada za kuwapatanisha ziligonga mwamba.


D'Banj alitweet kwa kusema "Pongezi kwa kaka yangu na producer bora barani Africa Don jazzy kwa kuanzisha Record Label, MAVIN RECORDS. Nakutakia kila lakheri"


Katika kuonesha upendo na shukrani kwa pongezi za D'Banj's Don Jazzy alijibu"Asante brother. Mungu akubariki"


Mapema wiki hii Don Jazzy alitangaza label yake mpya ambayo amemsainisha mwanadada Tiwa Savage na pia kuondoka na wasanii watatu waliokuwa Mo'Hits.

No comments:

Post a Comment