Thursday, May 10, 2012

Bracket kumshitaki msanii chipukizi wa Uganda kwa kuiba wimbo wao


Wanamuziki wa kundi la Bracket la Nigeria Ozioko Nwachukwu a.k.a Vast na Ali Obumneme wamepanga kumshitaki msanii anayechipukia kwa kasi nchini Uganda,  Ray wa Big Tym Crew kwa kuwaibia wimbo (Kukiuka sheria za haki miliki)

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa, wimbo wa Ray uitwao Kasenyanku, ambao unahit kinoma nchini Uganda ni kopi ya wimbo wao.

Wasanii hao walikuwa wanangalia video kwenye mtandao wa Youtube na kama bahati tu wakaiona video hiyo na walipousikiliza wakasikia unasound kila kitu kama wimbo wao uitwao Me & You.

Imedaiwa kuwa wanatafuta mwanasheria mzuri mjini Kampala ili kumshitaki msanii huyo. Gazeti la New Vision limedai kuwa baada ya kumpigia simu msanii huyo na kumwambia kinachoendelea alikuwa mdogo kama pilton na kuamua kuzima simu yake.

Ray hana cha kujitetea sababu trust us! wimbo huu ni copy and paste kila kitu kuanzia beat mpaka melody zake! Kazi ipo!

Haya sasa wanaijeria wameanza kucharuka na kutaka cha kwao, next bila shaka ni Jay Martins atakayetaka kuchukua chake kwa Ommy Dimpoz wa Baadaye! We are just saying!

No comments:

Post a Comment