Wewe ni promoter wa muziki na unataka kufanya show na Diamond? Then inabidi ujipange kwanza ili uepukane na mshtuko unaoweza kukusababishia pressure buree! kwa jibu atakalokupa.
Bila milioni 8 mezani kijana hapigi show mkoani kwako. Na hapo unaambiwa hakuna cha advance wala nini! Anakupa akaunti, unautuma mzigo wote na ndipo unapopata uhakika wa Diamond kuja kwenye show yako.
Kwa mapromoter wa kuungaunga mjini na wenye mitaji ya milioni mbili ndo waseme byebye kwa kijana coz the boy is expensive!
Mtangazaji wa Mbeya Fm Jackline Charles Marandu alipata idea ya kuandaa show na staa huyo wa ‘Mawazo’ na kuamua kumtwangia simu.
Jibu alilokutana nalo hakulitegemea “nimeishiwa nguvu huwezi amini yaani” alisema.
“Nimeongea naye mwenyewe kama nusu saa iliyopita (May 12) Nilitaka afanye show Mbeya ndiyo kanijibu hivyo. Sijajua yuko wapi kwa sasa. Nilitaka kumrekodi ila nikachelewa.Ukitaka show naye mkoani mfano Mbeya utamlipa shilingi milioni 8, utamlipia ndege yeye na utawalipia dancers wake 4 kwa basi”.
![]() |
| Jackline Marandu |
Kwa mikoa ambayo ndege haziendi ina maana Diamond ndo wamsahau kabisa kwa sasa? Ama ndo inabidi utafute private jet, makubwaaa!
![]() |
| Diamond na mshikaji wake Ommy Dimpoz kwenye Kili Awards Academy |
Kwa upande mwingine kauli ya Diamond inadhihirisha kuwa Bongo Flava sasa hivi ni biashara serious. Show kama Diamonds are forever na ile aliyopiga pale Dar Live mwezi uliopita vimemuongezea umaarufu msanii huyu anayejituma.
Swali ni Je! Jina lake la Diamond linasadifu uthamani alionao sasa?



No comments:
Post a Comment