Mafahari wawili hawakai zizi moja sio? Inakuaje kwenye zizi moja panapokuwa na mafahari zaidi ya wawili? Trouble!
Kwenye jumba la Big Brother mwaka huu pamejaa 'matozi' na 'maduu' ambao wengi wao kabla ya hata kuingia mjengoni walikuwa na majina makubwa na mshiko mrefu.
Mtu kama Prezzo kwa mfano! Inafahamika wazi kuwa anatoka kwenye familia bora. Hajaenda mle kwa njaa! Yuko njema tayari. Na hebu mchek mtoto Barbz wa Bondeni kwa Madiba. Kama haendi chooni vile! Sasa hebu pata picha yeye na Prezzo wazinguane! Patatosha?
Sasa mambo yashakuwa mambo. Prezzo si ameshamzingua Barbz!
Kivipi? Eti mtoto Barbz kammind Prezzo kumpa majina ya utani ya "Miss Mademoiselle" na "Tyra Banks.
Goldie wa Nigeria aliyeenda kumpoza Prezzo kwenye bustani aliambiwa kuwa maneno "Sorry" na "I love you" huwa hayatoki hovyo kwenye domo mdomo wake kirahisi na eti na kama ni $300,000 ndizo anazozitaka basi ajifunze (Barbz) kuongea vizuri.
"Wasichana wanafanya kazi zote na Barbz kazi yake ni kukaa tu na kujiangalia kwenye kioo,” Prezzo alilalamika, na kuongeza kuwa sio vizuri kwakuwa wote waliomo 'Upville' ni sawa.
It’s just getting started!

.jpg)
No comments:
Post a Comment