Linex aomba radhi kwa wanawake nchini kutokana na kibao alichompiga msichana wa video yake
Kutokana na kibao kikali alichomtandika msichana aliyeigiza kwenye video yake ya Aifola, Linex amewaomba radhi wanawake nchini kwa kile anachosema wasimfikiriE kuwa anachochea ukatili wa wanawake kwenye jamii.
Bonge la banzi
Kupitia Facebook Linex amesema:
“Naomba radhi kwa kila mwanamke Dunian kofi nililompiga vdeo gal wa kwenye aifola vdeo sikua nakusudia uchochezi wa mwanamke kupigwa na mwanaume wake natumai wanaume wenzangu mmenielewa lengo ilikua kutafuta uhalisia wa matukio kwenye video yangu #team mwanamke hapigwi analiwazwa na kubembelezwa.”
Akiongea na kipindi cha top 20 cha Clouds Fm leo ili kufafanua zaidi, msanii huyo wa Kigoma All Stars amesema hata mama yake baada ya kuina video hiyo alimpigia simu kumweleza kuhusu ‘kibao’ hicho.
No comments:
Post a Comment