Tuesday, July 10, 2012

Wazazi washikiliwa na polisi wa UAE kwa kumweka mtoto kwenye begi



Wanandoa wa nchini Misri wanashikiliwa na polisi kwa kosa la kuhatarisha uhai wa mtoto wao baada ya kumweka kwenye begi la nguo ili wawapite walinzi wa airport huko katika Umoja wa Falme za kiarabu (UAE).

Walinzi hao walimkuta mtoto huyo mwenye miezi mitano kwenye begi hilo dogo la nguo.

Polisi wamesema mtoto huyo aligunduluwa kwa X-ray kwenye uwanja huo wa ndege wa  Sharjah International Airport wakati wazazi wake walipokuwa wakisubiria kusafiri.



Hata hivyo mtoto huyo anaendelea vizuri.

Kwa mujibu wa polisi wa Sharjah, wanandoa hao waliwasili UAE ijumaa iliyopita lakini walizuiwa kuingia nchini humo kwasababu hawakuwa na visa ya mtoto wao.

Wazazi hao waliambiwa kusubiri kwa siku mbili hapo airport mpaka ofisi ya visa itakapofunguliwa ili visa ya mtoto wao iwezi kushughulikiwa.



Siku ya jumamosi baada ya uvumilivu kumshinda, baba wa mtoto huyo alimshawishi mke wake wamweke mtoto wao kwenye begi akiamini kuwa security hawatamuona.

"Tulishangaa sana. Hii ni mara ya kwanza kuona kitu kama hivi,” afisa wa polisi Abdel Rahman Shama aliiambia CNN. "Hata kama umekataa tamaa, utamwekaje mtoto kwenye begi?’

Wazazi hao wanashikiliwa na polisi nchini humo.

No comments:

Post a Comment