Kwa muda mrefu tumekuwa tukijiuliza kuwa ni lini Tanzania itafanya gospel kama ya Kenya? Kwa taarifa yako tu kuwa pamoja na kuwepo na muziki wa injili uliozoeleka kwa watu wengi Tanzania ambao huwa na mahadhi ya kwaya zaidi, Kenya wamepiga hatua kwa kufanya muziki wa injili unaowavutia vijana wengi. Ndo maana kuna nyimbo za gospel nchini Kenya zinawashawishi mpaka madj wa klabu kuzipiga.
Dunia ya leo imebadilika ambapo wapo vijana wanaondena na wakati lakini ni waumini wazuri kanisani na wengine wameokoka. Vijana hawa ni vigumu sana kuwakuta wakisikiliza nyimbo za wasanii kama Rose Muhando ama Bahati Bukuku nyumbani.
Si kwakuwa nyimbo hizo ni mbaya lahasha! Ni kwasababu sio aina yao ya muziki! Ndo maana wengi kama wakitaka kusikiliza gospel, basi watasikiliza za kiingereza ambazo huwa na mahadhi ya soft rock, rnb, country ama hip hop!
Hii ni kwasababu hapa Tanzania hakuna gospel ya aina hii, inayoweza kuwavutia vijana wanaondena na wakati. Ndo maana kwenye kichwa cha habari hapo juu tumesema video hii ya Monica kutoka Arusha inaweza kuleta mapinduzi.Wapo wanaojaribu lakini mara nyingi video zao ni za kawaida sana pengine ni kutokana na kipato kidogo.
Ni video kwaajili ya wacha Mungu lakini ni ya kijanja. Wimbo huu pamoja na video yake ndiyo inaweza kumshawishi kijana tunayemzungia hapo juu.
Ni wimbo ulioimbwa katika mahadhi ya rnb ambayo yanaweza yakamshawishi hata mtu asiyemuumini mzuri kukaa na kusikiliza hasa kama akiwa kijana ambaye husikiliza nyimbo zenye mahadhi ya rnb.
Kila kitu kimefanya na Nisher kwenye wimbo huu. Yeye ndiye mtunzi, mtayarishaji na ndiye aliyetengeneza video hii.
No comments:
Post a Comment