Jumapili iliyopita msanii chipukizi wa Nigeria, aliyejipatia umaarufu ndani ya kipindi kifupi Davido, aliperform kwenye Eviction show ya Big Brother Africa Stargame.
Ngoma aliyoperform inaitwa Dami Duro ambayo kwa sasa ni club banger matata sana barani Africa. Ni ngoma kali to be honest!
Tatizo letu linakuja kwenye performance hii ambayo tunaweza kuiita ya kitoto. Labda sisi tunasikia vibaya, lakini hata macho hayadanganyi tukionacho kwamba kijana alikuwa akisynch mwanzo mwisho.
Tunafahamu kuwa show za Big Brother hazisindikizwi na live band hivyo wasanii huimba kwa kutumia beat chorus. Yaani msanii anaimba live kwenye sehemu ya verse tu na zile back alizoweka studio ndo zinaweza kubaki kwenye beat kumsupport.
Lakini kwa show ya Davido masikio hayatudanganyi kuwa tunachosikia mwanzo hadi mwisho wa performance yake ni vocal tamu za studio na yeye akiruka ruka tu na mpambe wake.
Tena tunahisi mic zilikuwa zimezimwa kabisa sababu hasikiki akiimba chochote! Hakuna haya yoyoyoyo! Damn! Why holding a mic if you don't even sing!! Bahati yake ni kwamba ngoma ni kali, watu wanaipenda kwahiyo ilikuwa shangwe tu mjengoni na tena ukizingatia sound system ya nguvu iliyofungwa mle ndani, aahh ni raha tu.
Lakini mtindo huu unaoendekezwa na waandaji wa Big Brother una hasara kubwa kwa wasanii wenyewe. Davido ni msanii mkubwa kufanya performance kwa ‘kusynch’ (kujifanya unaimba wakati cd ya wimbo original inaimba).
Huo ulikuwa ni muda kwake kudhihirisha kuwa si msanii wa studio tu bali anaweza kufanya show kwa sauti yake halisi na watu bado wakaifurahia.
Pamoja na umaarufu wake, sisi tunasema hii ndio performance mbaya kabisa tangu show hizo zianze kwenye shindano la Big Brother.
No comments:
Post a Comment