Mtoto wa kiume wa rapper wa zamani Coolio, Grtis Ivey, 22, amehukumiwa kwenda jela karibu miaka minne kwa kosa la kukaba na wizi wa kutumia nguvu.
Ivey alitenda kosa hilo November 14, 2011 ambapo alimkaba mkazi mmoja mjini Las Vegas na kumpiga.
Katika tukio hilo Ivey alikuwa na bunduki na kusikindikizwa na changudoa aliyemsaidia kufanya uhalifu huo.
Atatumikia kifungo cha miaka 3.5 jela hadi miaka 10 kutegemea na huruma ya jaji.
Grtis Ivey ni mtoto wa kwanza wa Coolio. Jaji atatoa hukumu rasmi September 12.
No comments:
Post a Comment