Wednesday, July 11, 2012

Mazishi ya bibi yake: Rihanna ajiliwaza na beer



Akiwa amevaa gauni jeusi la kawaida tu lakini lililompendeza, jana Rihanna ameomboleza kifo cha bibi yake mpendwa, Dolly.

Mrembo na mwanamuziki huyo mwenye miaka 24, alihudhuria mazishi ya bibi yake kwao Barbados na ni wazi alikuwa na huzuni.


Muda huo Rihanna alitweet ujumbe wa kumuaga bibi yake “Get your beauty rest until I see you.”

Kabla ya kwenda kwenye mazishi, nyota huyo alitweet picha inayomwonesha akiwa ameshika bia na kuiwekea maneno, “I had to!!! Sorry granny”

No comments:

Post a Comment