Wednesday, July 11, 2012

Albam ya Chris Brown yakamata No.1 kwenye Billboard 200




Albam mpya ya Chris Brown Fortune imekamata nafasi ya kwanza leo jumatano kwenye chart ya Billboard 200 licha ya kushindwa kuwashawishi wakosoaji wa muziki wiki iliyopita.

"Fortune" imeuza kopi 134,000 katika wiki ya kwanza kwa mujibu wa  Nielsen SoundScan, ikiwa ni idadi ndogo ukilinganisha na albam yake ya mwaka jana, F.A.M.E. ambayo iliuza kopi 270,000 katika wiki ya kwanza na kukamata No. 1.

Hata hivyo albam ya Chris ndo albam mpya iliyoingia kwenye top 10.



No comments:

Post a Comment