Tuesday, May 8, 2012

Vanessa Mdee aja na Dume Challenge



Ni Mtangazaji/dj wa radio (Choice FM),mtangazaji wa TV (MTV VJ) mwanaharakati wa HIV/AIDS, mwanamitindo, mhariri na vyeo vingine vingi.

Vanessa Mdee aka Miss Dynamite ameendelea kuonesha kuwa kwa kufanya kazi kwa bidii na kutokata tamaa unaweza kufanikisha lolote.

Tangu mwaka 2007 Vee amefanikiwa kuiteka mioyo ya wengi. Akiwa na miaka 19 peke yake, Vanessa,mwanafunzi wa The Catholic University Of Eastern Africa aliibuka mshindi katika shindano la kumsaka mtangazaji mwakilishi wa Tanzania wa MTV na hatimaye kuungana na Carol and Kule kufanya kipindi cha Coca Cola Chart Express.

Na sasa baada ya kutumia mwezi mmoja kushoot reality show mpya iitwayo DUME CHALLENGE ameweza kutoa vipande vya behind the scenes show itakavyokuwa. Angalia kipande hicho kwa kuclick hapo chini.


Dume Challenge inayotayarishwa jijini Dar es Salaam itahusisha wanaume shupavu 12 ambao watakuwa wakichuana katika wiki 13 kumpata mshindi atakayeibuka na shilingi milioni 20.


Show yenyewe itaanza kurushwa mwezi ujao (June) katika kituo ch ITV.
Miongoni mwa washiriki katika kipindi hicho ni Gwasi, yule model aliyejizolea umaarufu katika tangazo maarufu la Tigo Longa Longa na anayeonekana akikimbia mbio kuwahi kupiga simu.

Kwa namna utayarishaji wake ulivyo, bila shaka Dume Challenge inakuja kuwa show kali kabisa kuwahi kutokea Tanzania.

No comments:

Post a Comment